RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI WAPYA NA VIONGOZI ALIOWATEUA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, July 3, 2018

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI WAPYA NA VIONGOZI ALIOWATEUA

Rais John Magufuli amewaapisha rasmi  viongozi mbalimbali aliowateua jana baada ya kufanya mabadiliko mafupi.

Akihutubia katika hafla hiyo Rais Magugfuli ameelezea mambo mbalimbali ambayo anayaona hayaendi sawa katika idara nyeti za serikali anayoiongoza.

Aidha Rais Magufuli amewataka viongozi aliowateua kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuwaletea wananchi walioichagua serikali yake maendeleo.

Awali akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania waziri mkuu kassim majaliwa amesema viongozi walioapishwa leo wanajukumu la kuwatumikia watanzania bila kuchoka.

Walioapishwa ni Kangi Lugola anayekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mwigulu Nchemba.

Wengine ni Profesa Makame Mbarawa aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Maji na umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwele aliyeteuliwa kuwa Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Wengine ni Thomas Mihayo anayekuwa Kamishna wa  Tume ya Uchaguzi(NEC), pamoja na makamishna wengine

Amos C Nyanduku
Loading...

No comments: