RAIS MAGUFULI, DKT MENGI WAMWINUA KIUCHUMI BINTI MLEMAVU MWENYE NDOTO ZA KUWA MUONGOZAJI FILAMU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, July 3, 2018

RAIS MAGUFULI, DKT MENGI WAMWINUA KIUCHUMI BINTI MLEMAVU MWENYE NDOTO ZA KUWA MUONGOZAJI FILAMU

Rais Dkt. John Magufuli amempatia msaada wa Tsh. Milioni 10, binti Wakonta Kapunda mwenye ulemavu wa miguu na mikono anayeandika kwa kutumia ulimi, ili zimsaidie kutimiza ndoto yake ya kuwa mwongozaji wa filamu (film director).

Rais Magufuli ametoa fedha hizo leo, wakati akizindua kitabu cha mfanyabiashara Dkt. Reginald Mengi kinachoitwa ‘I Can, I Must, I Will- The Spirit of Success’ chenye maudhui ya kumfundisha Mtanzania kujikwamua kutoka kwenye umaskini.

Awali akizungumzia kitabu chake Mwenyekiti Mtendaji wa iPP Dkt Reginald mengi amesema, lengo la kutunga kitabu hicho ni kuwawezesha wajasiriamali kutokata tamaa katika shughuli zao

Katika hatua nyingine Dkt Mengi amempatia dola elfu 20 Msichana Wakonta Kapunda baada ya kuibuka mshindi katika shindano la kuandika mchanganuo wa biashara linaratibiwa na Dkt Mengi

Wakonta alipata ajali na wanafunzi wenzake wa Kidato cha VI, katika Shule ya Wasichana Korogwe, Tanga mwaka 2012.

Loading...

No comments: