RC MAKONDA AWAFUNGA MIDOMO WALIOKUWA WAKIBEZA MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, July 14, 2018

RC MAKONDA AWAFUNGA MIDOMO WALIOKUWA WAKIBEZA MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema serikali ya awamu ya tano inaendelea kutekeleza Irani ya chama cha mapinduzi CCM kwa kufanya shughuli mbali mbali za maendeleo zenye kuleta tija kwa Taifa.
Makonda amebainisha hayo kwenye mkutano maalu m wa Halmashauri Kuu na wadau wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya mafanikio ya serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza irani ya uchaguzi ya CCM Kuanzia januari 2016 hadi 2018.
dha RC Makonda amesema serikali kwa kushirikisha wadau imefanikisha ujenzi wa Jengo la Mama na mtoto hospital ya Chanika, Amana, Jengo la Upasuaji Mwanayamala, jengo la wagonjwa wa dharura Temeke, Zoezi la upimaji afya Bure kila mwaka, ujenzi wa zahanati na vituo vya afya pamoja na kusimamia upatikanaji wa dawa, vifaa tiba pamoja na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.
Kwa upande wa sekta ya miundombinu ya barabara RC Makonda amesema serikali imefanikiwa kujenga barabara,mifereji na madaraja kupitia miradi iliyopo chini ya TANROAD, TARURA na DMDP jambo lililosaidia kupunguza kero kwa watumiaji wa barabara.


Pamoja na hayo RC Makonda ameeleza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. Magufuli imefanikiwa kuboresha mazingira ya kazi kwa jeshi la polisi kupitia ujenzi na ukarabati wa vituo vya polisi, kuwapatia magari, pikipiki, baiskeli na computer na kufanya polisi kuwa na morali ya kazi na kupungua kwa uhalifu.
Sekta nyingine ambazo zimetekelezwa kwa mkoa wa Dar es salaam kupitia ilani ya CCM ni pamoja na utawala bora, uchumi, kilimo, maji, kilimo, maliasili na utalii, mazingira, usafirishaji.
Amos C Nyanduk
Loading...

No comments: