RC MAKONDA KUPOKEA MWENGE WA UHURU KESHO. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, July 6, 2018

RC MAKONDA KUPOKEA MWENGE WA UHURU KESHO.

Mkoa wa Dar es Salaam siku ya kesho Jumamosi ya Julai 07 unatarajia kupokea Mwenge Uhuru utakaokimbizwa jijini humo kwa Muda wa siku Tano na kuzindua miradi mikubwa ya maendeleo zaidi ya 33.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema Mwenge huo utawasili kesho majira ya Saa 12 Asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere Terminal 1 ukitokea Pemba na baada ya kuupokea ataukabidhi kwa uongozi wa Wilaya ya Ilala kwaajili ya mbio na baada ya hapo utaenda Wilaya za Kigamboni, Kinondoni, Ubungo na kumalizia na Temeke.

Na Amos C Nyanduku

Loading...

No comments: