Tigo na TECNO wanaungana kuleta simu za kisasa kwa gharama nafuu. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, July 8, 2018

Tigo na TECNO wanaungana kuleta simu za kisasa kwa gharama nafuu.

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu aina ya Tecno S2 kwa mpiga picha Goodluck AMsola (kulia) aliyoshinda katika droo ndogo iliyofanyika wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe za simu kutoka Tigo na Tecno katika msimu huu wa Sabasaba. Katikati ni Afisa Mawasiliano wa Tecno, Eric Mkomoya.Ofa murwa kwa simu mpya za TECNO zenye intaneti bure kwa miezi sita toka Tigo

Dar es Salaam, 6 Julai 2018… Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania imeungana na TECNO wameungana kuwapa wateja fursa ya kumiliki kwa bei nafuu, simu janja zenye uwezo wa 4G  na intaneti bure kwa miezi sita kutoka Tigo.
Katika msimu huu wa Sabasaba, Tigo na TECNO wanakuletea simu za TECNO S2 kwa bei ya TSH 83,000, na TECNO R6 plus kwa bei pungufu ya TSH 195,000.

“Simu inayotumia laini mbili ya TECNO S2 pamoja na simu janja ya TECNO R6 plus zote zinakuja na ofa ya GB 2 za intaneti kwa miezi sita kutoka Tigo,’ Woinde Shisael, Meneja Mawasiliano wa Tigo alisema katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika Maonyesho ya Dar es Salaam ya Kimataifa ya Biashara  katika viwanja vya JK Nyerere jijini Dar es Salaam.

Shisael aliongeza kuwa,“Tigo wanaongoza mabadiliko ya maisha ya kidigitali. Tunalenga kuongeza matumizi ya simu janja nchini na kuhakikisha kuwa wateja wetu wote wanafurahia huduma bora zaidi ya kidigitali kupitia mtandao wetu mpana na wenye kasi ya juu zaidi wa Tigo.”

Akizungumzia ushirikiano huo, Eric Mkomoya, Afisa Habari wa TECNO alisema, “Simu zetu zinaweka viwango vipya vya ubora na raha ya matumizi. TECNO inaamini kuwa kila mteja anahitaji kupata bidhaa yenye viwango vya juu vya  ubora na umbo la kuvutia.
Mkomoya aliongeza kuwa “Pamoja na kutengeneza bidhaa za kuvutia zinazolenga kuongeza raha ya matumizi kwa wateja, tunatengeneza bidhaa madhubuti zenye uwezo wa kuboresha faida ya matumizi kwa maisha ya kila siku ya mteja..”
Simu zote zinapatikana katika banda la Tigo lilipo katika Maonyesho ya Dar es Salaam ya Kimataifa ya Biashara  pamoja na katika maduka yote ya Tigo nchi nzima.

MWISHO.

Loading...

No comments: