Ufaransa Yatinga Fainali Kombe La Dunia, Sasa Kuisubiri England Au Croatia Leo Saa tatu Usiku - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, July 11, 2018

Ufaransa Yatinga Fainali Kombe La Dunia, Sasa Kuisubiri England Au Croatia Leo Saa tatu Usiku

Timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ubelgjiji.

Bao pekee la beki wa kati anayeichezea FC, Barcelona, Samuel Umtiti limeifikisha fainali Ufaransa mnamo dakika ya 51 ya kipindi cha pili kwa kumzidi ujanja beki Marouane Fellaini kuuwahi mpira na kufunga kwa kichwa kupitia kona.

Matokeo hayo yanaifanya Ufaransa sasa kusubiri mshindi wa nusu fainali ya pili leo  baina ya England dhidi ya Croatia itakayopigwa majira ya saa 3 usiku.
Loading...

No comments: