Video: Mashabiki wa Juventus wamshangaza Ronaldo kwa mapokezi yao asubuhi ya leo - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, July 16, 2018

Video: Mashabiki wa Juventus wamshangaza Ronaldo kwa mapokezi yao asubuhi ya leo
Video: Mashabiki wa Juventus wamshangaza Ronaldo kwa mapokezi yao asubuhi ya leo

Hii leo siku ya Jumatatu, Cristiano Ronaldo amewasili Makao Makuu ya klabu ya Juventus tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha usajili wake akitokea Real Madrid ya Hispania.
Juventus imeposti kipande cha video ikimuonyesha mshambuliaji huyo akisalimiana na mashabiki wa klabu hiyo amboa walikuwa hapo muda wote kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Ronaldo ametua nchini Italia majira ya asubuhi hii leo siku ya Jumatatu baada ya kukamilisha uwamisho uliyoshangaza ulimwengu wa euro milioni 100 sawa na dola za Kimarekani milioni 116 akiachana na mabingwa wa kihistoria wa klabu bingwa barani Ulaya klabu ya Real Madrid.
Mshindi huyo maratano wa taji la Ballon d’Or  kwa sasa yupo Allianz Stadium kwaajili ya vipimo vya afya na mara baada ya tukio hilo atasaini kandarasi ya miaka minne na mabingwa hao wa  Serie A.

Loading...

No comments: