WAZIRI MBARAWA AKABIDHIWA RASMI OFISI, AWATAKA WATUMISHI WA IDARA YA MAJI KUONGEZA UFANISI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, July 4, 2018

WAZIRI MBARAWA AKABIDHIWA RASMI OFISI, AWATAKA WATUMISHI WA IDARA YA MAJI KUONGEZA UFANISI

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa leo amekabidhiwa rasmi ofisi yake katika wizara ya maji jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku mbili baada ya kuapishwa na Rais Magufuli kuwa Waziri wa Wizara hiyo.
Akizungumza na watumishi wa wizara hiyo  jijini Dar es Salaam Mbarawa amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuisimamia wizara ya maji huku akiongeza kuwa amepata nafasi ya kwenda kubadilisha  maisha ya watanzania.
Aidha Prof  Mbarawa ameweka wazi mambo matatu muhimu ambayo anatamani yapewe kipaumbele katika wizara ya maji ili taasisi hiyo iweze kwenda mbali zaidi, huku akilenga matumizi mazuri ya maji, huduma kwa wateja pamoja nakutaka kuongeza idadi ya wateja hadi kufikia laki nane na nusu.
Mbarawa amesema kuwa wizara ya maji ni Taasisi kubwa na kutoa agizo kwa viongozi wa wizara hiyo kuhakikisha wanaanza kutumia mita za kielektroniki  na kuachana na mita za zamani
Loading...

No comments: