PROF MAJI MAREFU AAGWA NA WABUNGE KUZIKWA KWAO KOROGWE KESHO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, July 4, 2018

PROF MAJI MAREFU AAGWA NA WABUNGE KUZIKWA KWAO KOROGWE KESHO


Waziri Mkuu Kasim Majaliwa leo amewaongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Korogwe vijijini Steven Ngonyani aliyefiriki Dunia Julai 2, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)

Viongozi wengine waliohudhuria katika ibada hiyo ya kuuaga mwili wa Marehemu Maji Marefu katika Viwanja vya Karimjee kutoa heshima za mwisho ni Spika wa Bunge Job Ndugai na Naibu wake Tulia Ackson.

Wengine ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, mawaziri na wabunge mbalimbali.

Akitoa salamu za serikali katika shughuli hiyo Waziri Majaliwa ameitaka familia ikiwemo wake wa marehemu kuwa watulivu na wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Akizungumza kwa niaba ya kambi  ya upinzani Mbunge wa Vunjo James Mbatia amesema, Kambi hiyo imesikitishwa na kifo cha Majimarefu kwani alikuwa mpambanaji, mcheshi na mpenda watu bila kubagua chama.

Na Amos C Nyanduku

Loading...

No comments: