NDEGE YA BOEING 787 YAPOKELEWA MWANZA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, July 30, 2018

NDEGE YA BOEING 787 YAPOKELEWA MWANZAyake ikitokea Dar kwenda Mwanza na kupokelewa na umati mkubwa wa wananchi wakiongozwa na waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe akiambatana na viongozi mbalimbali wa serikali.

Ndege hiyo imewasili Mwanza majira ya saa nne asubuhi ikiwa na abiria zaidi ya 260 ikiwa ni safari yake ya kwanza hapa nchini,Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe amesema kuanza kwa safari hiyo inaongeza matumaini ya Serikali kununua ndege zingine.


John Mongela ni mkuu wa mkoa wa Mwanza amesema jitihada zinazofanywa na serikali zinatakiwa kuungwa mkono na watanzania wote huku akiahidi kuendelea kutengeneza miundombinu ya uwanja wa Mwanza.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Mwanza Anthony Diallo na katibu mwenezi ccm Taifa Hamphrey Polepole wamesema ujio wa ndege hiyo ni utekelezaji wa ilani ya chama hicho pamoja na watanzania kukubali kulipa kodi.


Nao baadhi ya abiria na wananchini amefurahishwa na usafiri wa ndege hiyo.

Ndege hiyo inatarajiwa kufanya safari zake katika mikoa ya Mwanza,Dar na Kilimanjaro.
Loading...

No comments: