BENKI YA NIC YAZINDUA KADI ZA VISA ZIITWAZO 'NIC VISA MOVE DEBIT CARD' TAWI LA OHIO JIJINI DAR ES SALAAM LEO. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, August 28, 2018

BENKI YA NIC YAZINDUA KADI ZA VISA ZIITWAZO 'NIC VISA MOVE DEBIT CARD' TAWI LA OHIO JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NIC Bw. Mick Karima akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kadi mpya ya visa waliyo ianzisha na inayokwenda kwa jina la 'NIC Visa Move Debit Card' katika Tawi lao la Ohio leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NIC Bw. Mick Karima (kulia) akiwa na Bw. Deepak Doshi ambaye ni mteja wa kwanza kutumia huduma ya 'NIC Visa Move Debit Card'(wa tatu kutoka kushoto) pamoja na Mkuu wa kitengo cha Masoko kutoka Benki ya NIC Bi. Natasha Cathles wakionesha mfano wa kadi hiyo ya Visa.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NIC Bw. Mick Karima akitoa neno la ufunguzi rasmi wa Kadi yao mpya ya Visa inayokwenda kwa jina la 'VISA MOVE DEBIT CARD'. Wakati wa uzinduzi huo Bw. Mick Kirima alisema kuwa "Uzinduzi huu unaashiria hatua muhimu sana kwa Benki ya NIC kadri tunavyoendelea kuwapa wateja wetu huduma mbalimbali ambazo zinaboresha maisha yao, Benki inaendelea kutafuta ufumbuzi wa kuwaboreshea wateja matumizi ya huduma zetu na kwenda mbele tutaanzisha huduma za unafuu zaidi".
 Bw. Imitiaz Esmail Meneja wa Usimamizi wa Fedha na Bidhaa wa Benki ya NIC akitoa maneno ya utangulizi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kadi mpya ya 'NIC Visa Move Debit Card', ambapo alizungumzia bidhaa mbalimbali na huduma ambazo wanazitoa katika Benki hiyo ambayo inaendelea kukuwa kwa kasi kulingana na mabadiliko ya Teknolojia. 
Mkuu wa kitengo cha Fedha wa Benki ya NIC  Bw. Msafiri Kibebeti akizungumzia maswala mbalimbali yanayohusiana na fedha katika Benki hiyo, ambapo alisema kuwa mpaka sasa kwa upande wa Tanzania wanamatawi matano Arusha, Mwanza na Dar es Salaam yakiwa matawi matatu (Ohio, Samora na Kariakoo). "Benki ya NIC Tanzania inajivunia kua kituo kimoja cha huduma mbali mbali za kifedha, akaunti binafsi na za biashara, akaunti za kuhifadhi fedha za biashara, bima ubadilishaji wa fedha za kigeni na huduma za kibenki kwa taasisi" alisema Msafiri.
Mteja wa Kwanza kabisa kuchukua fedha kupitia 'NIC Visa Move Debit Card' Bw. Deepak Doshi akiendelea kutoa fedha katika ATM iliyopo Ohio ndani ya jengo la Golden Jubilee Towers. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NIC Bw. Mick Karima.
  Bw. Deepak Doshi ambaye ni mteja wa kwanza kutumia huduma ya 'NIC Visa Move Debit Card' akitoa fedha zake.
Bw. Deepak Doshi ambaye ni mteja wa kwanza kutumia huduma ya 'NIC Visa Move Debit Card'akiwa amekamilisha zoezi la kutoa fedha zake, ikumbukwe kuwa kadi hiyo inamuwezesha mteja kuchukua fedha katika ATM yoyote yenye VISA popote Duniani pia anaweza kufanya manunuzi ki elekroniki.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NIC Bw. Mick Karima (kushoto) akimpongeza Bw. Deepak Doshi ambaye ni mteja wa kwanza kutumia huduma ya 'NIC Visa Move Debit Card' baada ya kutoa fedha zake.
Wateja wa Benki ya NIC pamoja na wafanyakazi wa Benki hiyo wakiwa katika hafla fupi ya uzinduzi wa 'NIC Visa Move Debit Card'
 Burudani ikiwa inaendelea wakati wa uzinduzi wa 'NIC Visa Move Debit Card' katika Tawi la Ohio jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja ya wafanyakazi wa Benki ya NIC.
Picha na Fredy Njeje/ Mwanaharakati Mzalendo

Loading...

No comments: