Bobi Wine aachiwa kwa dhamana - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, August 28, 2018

Bobi Wine aachiwa kwa dhamanaMahakama Kuu ya Gulu nchini Uganda imempatia dhamana Mbunge wa Kyadondo Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine katika kesi yake inayomkabili ya uhaini.

Dhamana hiyo ni baada ya Mbunge huyo na wenzake 34 waliofika  mahakamani mjini Gulu kuomba mahakama iwaachilie kwa dhamana leo asubuhi wakiwa na mawakili wao.

Jaji wa mahakama ya Gulu Stephen Mubiru alikubali maombi ya dhamana hiyo, baadhi ya watu walioshtakiwa pamoja na mbunge huyo ni Mbunge wa kuteuliwa Kassino Wadri, Mbunge wa Jinja Magharibi,Paul Mwiru,Mbunge wa Ntungamo Gerald Karuhanga, na aliyekuwa mstaafu wa Makindye Mike Mabikke.

Mbunge huyo mpaka kukamatwa kwake na kushikiliwa kwenye gereza la jeshi la Makindye nchini humo alidaiwa kukamatwa akiwa na risasi na kuushambulia msafara wa Rais Yoweri Museveni kwa mawe. Lakini Bobi Wine ameonekana akitembea kwa magongo na kuzua masikitiko kwa wafuasi wake mahakamani hapo.

Loading...

No comments: