CBA BANK YAWAINUA WAJASIRIAMALI WADOGO NA MIKOPO YA M-PAWA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, August 31, 2018

CBA BANK YAWAINUA WAJASIRIAMALI WADOGO NA MIKOPO YA M-PAWA


CBA ikiwa moja ya benki inayoheshimika kwa huduma za kibenki ambayo imeendelea kutumia teknolojia kuboresha huduma zake kufuatia mapendekezo ya thamani ya huduma zinazotolewa kwa wateja wake. Ikishirikiana na Vodacom Tanzania, kama shirika la mawasiliano ya simu wameendelea kuboresha, ambayo inatarajiwa kuimarisha soko la Watanzania haswa wale wanaotegemea huduma za kibenki kupitia simu za mkononi.


Kupitia huduma ya M-Pawa, Watanzania ambao tayari wanatunia M-PESA wanaendelea kufurahia huduma za kibenki kwa wakati, huku mamia ya wajasiriamali na wafanyabiashara wadogowadogo wakinufaika na huduma hiyo inayowawezesha kupata mikopo midogomidogo papo kwa papo kupitia simu zao za mikononi.Kulingana na maendeleo ya kidijitali, M-Pawa imeonekana kuwa chaguo kubwa la wengi, kitu ambacho kimeipa huduma hii urahisi wa kupatikana na watumiaji wakati wowote. Ukiacha huduma nyingine zenye milolongo mirefu katika kujiunga na kutumia, hii unaweza kujiunga kirahisi ukiwa na simu yako tu kama mtumiajia wa M-PESA.
Mmoja wa wajasiriamali na mtumiaji wa M-Pawa, Shilole ameonyesha kunufaika kwake na mikopo ya M-Pawa ambayo ni rahisi, ya kuaminika na yenye gharama nafuu akiongezea kuwa pia M-Pawa imemuwezesha kuweka akiba ndogo ambayo mpaka sasa anaendelea kuweka na ameweza kukuza biashara yake kwa kiasi Fulani kama mpambanaji.

Shilole akiwa kama mtumiaji mkubwa wa M-Pawa amesema huduma hii imemsaidia kufikia malengo yake huku akielezea faida chungu nzima anazopata ambazo ni pamoja na urahisi wa kupata huduma za kibenki akitumia simu yake mkononi, mlolongo mfupi na huduma salama na ya haraka, hakuna kiwango cha chini kujiunga, hakuna ada ya malipo na viwango vyake vya riba ni vya kuridhisha.


Kwa ujumla, M-Pawa inakuwezesha kuweka akiba kwa usalama katika simu yako, ikikuwezesha kukamilisha malengo yako. Ili kupata mkopo kupitia M-Pawa, unahitaji kuwa umetumia M-PESA angalau kwa miezi 6. Pia unaweza kuchukua mkopo wakati wa dharura au unapohitaji kukuza biashara yako na kulipa kama inavyohitajika ndani ya muda ulioainishwa. Anza leo kufurahia huduma za M-Pawa piga, *150*00#, halafu chagua M-Pawa namba 5

Loading...

No comments: