JK AFIKISHA SALAMU ZA PONGEZI ZA JPM KWA RAIS MNANGAGWA WA ZIMBABWE


 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Zimbabwe Mhe.  Emmerson Dambudzo Mnangagwa zilizofanyika leo Jumapili Agosti 26, 2018 katika uwanja wa michezo mjini Harare. Katika safari hiyo Dkt. Kikwete aliambatana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Bw.. Philip Mangula akiwa na Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP) Bw. John  Momose Cheyo kama wanavyoonekana pichani wakiwa na mazungumzo na Rais Mnangangwa jijini Harare baada ya sherehe za kuapishwa.
Rais Mnangagwa akiwa na mazungumzo na Dkt. Kikwete.
Dkt. Kikwete, akisalimiana na Katibu Mtendaji Mkuu wa SADC,Dr. Stergomena L. Tax kwenye uwanja wa michezo mjini Harare, Zimbabwe wakati wa sherehe za kuapishwa kwa Rais Mnangangwa.
JK akiwasili kwenye uwanja wa michezo wa Harare tayari kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais Emmerson Mnangagwa.

Post a Comment

0 Comments