MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA KILELE CHA SHEREHE YA WAKIZIMKAZI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, August 14, 2018

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA KILELE CHA SHEREHE YA WAKIZIMKAZI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi kombe Nahodha wa Timu ya Wavuta Kamba ya Wanawake ya Kizimkazi Dimbani Bi. Nasma Khamis mara baada ya kuibuka washindi dhidi ya timu ya Kizimkazi Mkunguni ikiwa sehemu ya sherehe ya siku ya Wakizimkazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatibu Hassan wakiangalia mkoba wa wanawake uliosanifiwa na ukili waliotembelea maonyenyo ya wanawake na vijana wajasiriamali wakati wa kilele cha sherehe ya Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika Kizimkazi Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini Unguja. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Kundi la Kusini Star likitumbuiza wimbo maalum wa kujali haki za mtoto haswa wa kike wakati wa kilele cha sherehe ya Siku ya Wakizimkazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa wilaya ya Kusini kwenye kilele cha sherehe ya Siku ya Wakizimkazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Timu wa Wavuta Kamba ya Wanawake ya Kizimkazi Dimbani waangalia mchezo huo baada ya kuishinda timu ya Kizimkazi Mkunguni kwenye mchezo  uliochezwa wakati wa kilele cha sherehe ya Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika kizimkazi Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini Unguja. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Wakazi wa Kizimkazi wakipimana msuli kwenye mchezo wa kuvuta kamba ikiwa sehemu ya kilele cha sherehe ya Wakizimkazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) .

Loading...

No comments: