Mfanyabiashara Davis Mosha akamatwa na Askari wa Uhamiaji


Mfanyabiashara Davis Mosha alikamatwa Agosti Mosi, 2018 kwa madai ya kuwazuia askari wa Idara ya Uhamiaji kutekeleza majukumu yao na bado anaendelea kushikiliwa kwa hatua zaidi.

Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ali Mtanda amesema Mosha aliwashambulia askari hao na kumnyang’anya mmoja wao simu ya mkononi baada ya kufika katika jengo la Delina lililopo Sinza Mori.

“Askari walifika kwenye majengo hayo na kujitambulisha kwa mlinzi na moja kwa moja walionyeshwa ofisi za meneja. 
"Wakati wakifanya mazungumzo ya kikazi na meneja huyo, ghafla akatokea Mosha na kuanza kuwafokea, kisha kuwashambulia na kumnyang’anya askari mmoja simu yake.” –Mtanda
Amesema alichofanya Mosha ni kinyume cha sheria ya uhamiaji namba 54 kifungu cha 45 kipengele 1 F, kinachozungumzia kumzuia ofisa wa uhamiaji kufanya kazi yake ya ukaguzi.

Mtanda amesema bado wanamshikilia Mosha kwa uchunguzi zaidi na kama kuna hatua nyingine zitafuata watatoa taarifa.

Post a Comment

0 Comments