RC MAKONDA ATAKA MALI ZA UMMA ZILIZOTAIFISHWA NA WAJANJA KUREJESHWA MARA MOJA. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, August 4, 2018

RC MAKONDA ATAKA MALI ZA UMMA ZILIZOTAIFISHWA NA WAJANJA KUREJESHWA MARA MOJA.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo Kuunda Timu ya kufanya ukaguzi wa Mali zote za serikali zilizotaifishwa na wajanja ikiwemo maeneo ya wazi, Nyumba za umma na kubainisha mikataba yote mibovu inayoinyonya serikali.

RC Makonda ametoa agizo hilo leo wakati wa hafla ya kuwakaribisha wakuu wapya wa wilaya za Kinondoni na Kigamboni, Katibu Tawala Mkoa na kuwaaga wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ambapo amemuagiza katibu tawala kuhakikisha anakamilisha ripoti kabla ya September 03 mwaka huu.
Aidha RC Makonda amewataka watendaji kuhakikisha wanasimamia ipasavyo suala la ukusanyaji wa mapato na kuangalia chanzo kilichopelekea Mkoa huo kutofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato pamoja na kufanyia kazi kasoro zilizojitokeza.
Pamoja na hayo RC Makonda amemtaka katibu tawala kupanga safu mpya ya utendaji kazi ili kuhakikisha wanatatua kero za wananchi ambapo ametaka kuanza na idara ya ardhi, Biashara, Usafi, Mapato na michezo ambazo bado hazijamridhisha kiutendaji kazi.
Hata hivyo RC Makonda amewasihi viongozi walioteuliwa kuchapa kazi ili kuenda sambamba na kasi ya Rais Dkt.John Magufuli aliewaamini na kuwateua.

ACN
Loading...

No comments: