NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MH. JAPHET HASUNGA AZINDUA JITIHADA ZA TANZANIA KUUNGANA NA NCHI NYINGINE ZA AFRIKA KATIKA KUHIFADHI NA KUENDELEZA HIFADHI ZA MISITU,ULIOFANYIKA MSITU WA KAZIMZUMBWI , KISARAWE-PWANI. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, August 14, 2018

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MH. JAPHET HASUNGA AZINDUA JITIHADA ZA TANZANIA KUUNGANA NA NCHI NYINGINE ZA AFRIKA KATIKA KUHIFADHI NA KUENDELEZA HIFADHI ZA MISITU,ULIOFANYIKA MSITU WA KAZIMZUMBWI , KISARAWE-PWANI.

Mh. Japhet Hasunga (MB), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii pamomoja na Mh. Jokate Mwengelo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kwa pamoja wakipanda mti katika uzinduzi wa jitihada za Tanzania kuungana na nchi zengine za Afrika katika kuhifadhi misitu, tukio lililofanyika katika Msitu wa Kazimzumbwi Wilaya ya Kisarawe-Pwani.
Mh. Japhet Hasunga (MB), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa jitihada za Tanzania kuungana na nchi zengine za Afrika katika kuhifadhi misitu, tukio lililofanyika katika Msitu wa Kazimzumbwi Wilaya ya Kisarawe-Pwani.
Katibu Tawala Wilaya ya Kisarawe ndugu Mtela Mwampamba akitoa utambulisho kwa viongozi mbalimbali wananchi pamoja na wadau wengine waliofika katika uzinduzi huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwengelo akitoa salam zake wakati wa uzinduzi wa jitihada za Tanzania kuungana na nchi zengine za Afrika katika kuhifadhi misitu. Katika salam zake alisema kuwa Wilaya ya Kisarawe imezungukwa na misitu minne ya hifadhi ya Serikali ambayo ni Ruvu Kusini, Masanganya, Pugu na Kazimzumbwi na kuwa msitu wa Pugu na Kazimzumbwi ina wanyama na mimea ambayo haipatikani Tanzania na Duniani kwa ujumla jambo linalofanya kuwe sehemu muhimu kwa ajili ya watalii wa ndani na wa nje pia.
Mwakilishi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Ndugu. Alawi Haji Hija akitoa salam zake wakati wa uzinduzi wa jitihada za Tanzania kuungana na nchi zengine za Afrika katika kuhifadhi misitu.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya  Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo, akitoa maelezo mafupi kuhusu ahadi ya Nchi chini ya (AFR100 Initiative), alisema kuwa mkusanyiko wa wananchi, wahifadhi,wakuu wa taasisi za kiraia, NGO na CSO’s, Taasisi Mbalimbali za Serikali wote wana nia moja ya kuhifadhi rasilimali za misitu, Nyuki wanyama pori na rasilimali za Bahari, kuitikia mwito wa Dunia wa kuhifadhi misitu. Aliongeza kuwa Tanzania ni Miongoni mwa nchi ambazo zimeonesha nia ya kushirikiana na Dunia kuhifadhi misitu yake na Africa imeweka nia hiyo katika mkakati maarufu kama AFR100, ni nia ya Afrika kuhifadhi eneo la  misitu linalokaribia au kuzidi Hekta milioni mia moja kufikia mwaka 2030.
Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu,Sera na Mawasilino wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Ardhi Bi. Albina Burra katika salam zake alisema kuwa kwa kuwa wao ni wapangaji wa matumizi ya ardhi ambapo misitu ni eneo la matumizi ya ardhi na wanamaeneo makubwa ya wanyamapori na maeneo ya uoto. Alimalizia kwa kusema kuwa Tume inajukumu la kuhakikisha kila mtumiaji wa ardhi anapata ardhi ya kutosha na bila kusababisha migogoro na mwenzake pia bila kuharibu lasirimali za mazingira au ardhi yenyewe, "Tume ipo bega kwa bega na watu wa misitu kwa kuhakikisha kuwa misitu inalindwa kwa ajili ya manufaa ya viumbe hai na vitu vingine vinavyoendana na Bionuai" alisema Burra.
 Mkurugenzi Mkazi WWF Tanzania Dkt. Amani Ngusaru akitoa salam zake wakati wa uzinduzi wa jitihada za Tanzania kuungana na nchi zengine za Afrika katika kuhifadhi misitu.
Kamishna wa Skauti Tanzania Ndugu. Abdulkarim Shah, akitoa salam zake pia kuahidi kushirikiana kwa karibu katika kuutunza msitu huo.
 Meneja wa TFS Kisarawe Elias Mwaijele, Amemshukuru Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Japhet Hasunga kwa kuhudhuria katika  uzinduzi huo na kusema kuwa juhudi kubwa zimefanyika tangu mwaka jana kuwaondoa watu waliovamia misitu ili isiendelee tena kuharibiwa.
Mh. Japhet Hasunga (MB) Naibu waziri wa Maliasili na Utalii (wa pili kutoka kushoto) akitoa rasmi ahadi na kusema kuwa "Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania inaungana na nchi zingine za Afrika katika juhudi za kuhifadhi eneo la Hekta milioni mia moja (AFR100) KWA KUAHIDI KUHIFADHI HEKTA MILLION 5.2 IFIKAPO MWAKA 2030. Hii inamaanisha tutazuia kupotea/kuharibiwa kwa misitu yetu kiasi cha hekta 5,159,000ha Tanzania bara na hekta 25,190 kwa upande wa Zanzibar) ifikapo mwaka 2030)." 
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya  Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo(Kulia) na Mkurugenzi Mkazi WWF Tanzania Dkt. Amani Ngusaru(Kushoto) wakisaini Mkataba kati ya WWF na TFS kwa ajili ya kusaidia kulinda na kuhifadhi msitu wa Kazimzumbwi,Vikindu na Ruvu Kusini.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya  Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo(Kulia) na Mkurugenzi Mkazi WWF Tanzania Dkt. Amani Ngusaru(Kushoto) wakipena mikono baada ya kusainishana mkataba huo.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya  Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo(Kulia) na  Mkurugenzi Mkazi WWF Tanzania Dkt. Amani Ngusaru(Kushoto) wakionesha wananchi na wadau wengine mkataba huo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya  Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo akipanda mti katika uzinduzi wa jitihada za Tanzania kuungana na nchi zengine za Afrika katika kuhifadhi misitu, tukio lililofanyika katika Msitu wa Kazimzumbwi Wilaya ya Kisarawe-Pwani.
 Mwakilishi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Ndugu. Alawi Haji Hija akipanda mti katika uzinduzi wa jitihada za Tanzania kuungana na nchi zengine za Afrika katika kuhifadhi misitu, tukio lililofanyika katika Msitu wa Kazimzumbwi Wilaya ya Kisarawe-Pwani.
 Mkurugenzi Mkazi WWF Tanzania Dkt. Amani Ngusaru akipanda mti katika uzinduzi wa jitihada za Tanzania kuungana na nchi zengine za Afrika katika kuhifadhi misitu, tukio lililofanyika katika Msitu wa Kazimzumbwi Wilaya ya Kisarawe-Pwani.
 Kamishna wa Skauti Tanzania Ndugu. Abdulkarim Shah akipanda mti katika uzinduzi wa jitihada za Tanzania kuungana na nchi zengine za Afrika katika kuhifadhi misitu, tukio lililofanyika katika Msitu wa Kazimzumbwi Wilaya ya Kisarawe-Pwani.
Watu mbalimbali wakiwa kayika  uzinduzi wa jitihada za Tanzania kuungana na nchi zengine za Afrika katika kuhifadhi misitu, tukio lililofanyika katika Msitu wa Kazimzumbwi Wilaya ya Kisarawe-Pwani.
(Picha na Fredy Njeje )

Loading...

No comments: