RMO KAGERA ATAMANI MAGUFULI AONGOZE MILELE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, August 25, 2018

RMO KAGERA ATAMANI MAGUFULI AONGOZE MILELE


 Mganga Mkuu wa  Mkoa wa Kagera, Marko Mbata, akizungumza na waandishi wa habari mjini Bukoba mkoani Kagera jana, kuhusu kuhimarika kwa upatikanaji wa dawa mkoani humo ambapo alisema anatamani Rais Magufuli aendelee kuongoza nchi milele. 
Mfamasia wa mkoa huo, Pyuza Daniel akizungumza kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale, Kagera

MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Marko Mbata ameishukuru Serikali kwa kutenga bajeti kubwa ya dawa nchini ambayo imewezesha upatikanaji wa dawa kuimarika nchini ambapo kwa sasa upatikanaji wa dawa mkoani Kagera umefikia asilimia tisini na nane.

Mbata alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na ambao wapo ziarani mkoani Kagera kuangalia taratibu za usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye vituo vua kutolea huduma za afya mkoani Kagera. 

"Kwa kazi kubwa ya kuongeza bajeti ya dawa tangu alipoingia madarakani, natamani Rais Magufuli angeendelea kuongoza milele bila kufikia ukomo, kwani hii imeboresha kwa kiasi kikubwa sana hali ya upatikanaji wa dawa nchi nzima" alisema Mbata.

Amesema kwa wao kama wataalamu, walikuwa wakikwazika sana miaka ya nyuma pale mwananchi alipokuwa anakuja kupata matibabu na kukosa dawa, hivyo kwa hali ya sasa wanawahudumia wananchi vizuri na malalamiko ya wananchi yamepungua.

Ameipongeza MSD kwa kuweza kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji na kubadilisha vifungashio vya dawa kutoka kwenye makopo na kuziweka kwenye blister. 

Katika hatua nyingine Dkt. Mbata aliishukuru MSD kwa kujenga kituo cha mauzo wilayani Muleba kwani imewarahisishia watoa huduma wa afya kuwa karibu zaidi na MSD tofauti na ilivyokuwa awali walipokuwa wanapata huduma kutoka Mwanza.

Kwa upande wake mfamasia wa mkoa huo, Pyuza Daniel alisema licha ya maeneo ya vituo vya afya na zahanati yanapatikana visiwani,lakini kwa kushirikiana na MSD, wananchi na halmashauri dawa zimekuwa zikiwafikia walengwa kwa wakati.

"Kwa kweli lazima niwapongeze MSD kwa kazi kubwa wanayoifanya kwani sasa hivi wameboresha huduma, kikubwa waongeze idadi ya dawa ambazo zinakosekana kwenye orodha ya dawa ya sasa ili mgonjwa akifika kutibiwa kwenye aweze kuzikuta" alisema Daniel.
Loading...

No comments: