‘RYTHM’ ya QNET kugusa maisha ya jamii za wasiojiweza. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, May 27, 2018

‘RYTHM’ ya QNET kugusa maisha ya jamii za wasiojiweza.Wakala wa kampuni ya QNET wkitoa msaada wenye thamani ya zaidi ya milioni 9 kwa kituo cha watoto yatima cha Maunga mapema mwaka huu jijini Dar es salaam.


QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja inaamini katika maendeleo ya mtu binafsi na jamii kupitia kutengeneza fursa na inasisitizia falsafa hii katika biashara zake na katika shughuli zake za uwajibikaji kwa jamii.
Falsafa hii inatangazwa vyema zaidi kupitia kitengo cha kampuni cha uwajibikaji kwa jamii, RYTHM Foundation. RYTHM inasimama kama kifupisho cha Raise Yourself To Help Mankind, na kinajikita katika kanuni kwamba mtu anahitaji kujiwezesha yeye mwenyewe kwanza ili aweze kusaidia wengine kunyanyuka.  
Foundation hii imeandaliwa kwaajili ya kutoa elimu, kuhamasisha na kufanya kazi na wengine kutengeneza maisha mazuri ya baadae ya wale wenye uhitaji. Inagusa dhamiri ya jamii na inatoa ukumbusho wa umuhimu wa kuleta tofauti katika maeneo ya kazi, jamii au umma kwa ujumla.
Tanzania ilikuwa miongini mwa nchi 13 za kiafrika ambako QNET iliungana na IRs kuleta shangwe kwa jamii mbalimbali za watu wasio na uwezo, wakati wa sikukuu za hivi karibuni za mwezi mtukufu wa ramadhani.


MWISHO//

Loading...

No comments: