Serikali Yatoa Ajura kwa Walimu 2160 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, August 20, 2018

Serikali Yatoa Ajura kwa Walimu 2160

Serikali imatoa ajira kwa watumishi 2,160 katika shule za sekondari nchini ambapo kati yao waalimu 1900 ni wa masomo ya sayansi na hisabati.

Akizungumza leo jumatatu Agosti 20,2018 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amesema kati ya watumishi hao walioajiriwa 100 ni waalimu wa lugha na 160 ni fundi sanifu maabara.

Amesema watumishi hao wanatakiwa kuripoti katika ofisi za wakurugenzi wa halmashauri zilipo shule walizopangiwa kuanzia Agosti 23,2018 hadi Septemba 5,2018.

“Watumishi hao wanatakiwa kuripoti kwa muda huo wakiwa na vyeti halisi vya taaluma vya kidato cha nne na kidato cha sita, vyeti halisi vya kitaalam vya mafunzo ya ualimu vya ngazi husika pamoja na cheti cha kuzaliwa, na hatimaye kwenye shule walizopangiwa” amesema Jafo.

Hata hivyo, Jafo amewataka waajiriwa hao kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi na si makao makuu ya halmashauri ili kuomba kuhamishiwa vituo vya kazi.

“Mwajiri yeyote atakayechukua posho ya kujikimu kisha asiripoti kwenye kito chake cha kazi serikali itamchukulia hatua za kinidhamu,” amesema Jafo

Jafo ametumia nafasi hiyo kuwataka wakurugenzi wa halmashauri zenye vituo vya kazi walizopangiwa watumishi hao kuwapokea na kwa kufuata taratibu zote na kanuni za utumishi.


Loading...

No comments: