TAMASHA LA KWANZA LA MICHEZO LA AFRIKA MASHARIKI LAZINDULIWA JIJINI BUJUMBURA, BURUNDI. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, August 17, 2018

TAMASHA LA KWANZA LA MICHEZO LA AFRIKA MASHARIKI LAZINDULIWA JIJINI BUJUMBURA, BURUNDI.

Brigadia  Generali Mary Hiki akizungumza na wanamichezo kutoka (Tanzania hawapo pichani) washiriki wa Tamasha la Kwanza la Michezo la Afrika Mashariki linaloendelea jijini Bujumbura, Burundi. Brigadia Generali Hiki ambaye anahudumu katika Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi alizungumza na wanamichezo hao kwaniaba Kaimu ya Balozi.
Tamasha hili linalofanyika kwa mara ya kwanza nchi Burundi limetokana na maagizo ya Mkutano wa 35 wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki.

Tamasha hili lenye kauli mbiu "kujenga Jumuiya ya Afrika Mashariki na amani kupitia michezo" linafanyika kuanzia terehe 16 hadi 30 Agosti, 2018. Washiriki zaidi 1000 kutoka nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki watashiriki kwenye michezo mbalimbali ya tamasha hili.

Tanzania imewakilishwa na jumla ya wanamichezo 58 ambao watashiriki katika michezo ya mpira wa pete, mpira wa miguu, riadha na karatee.

Tamasha hili limefunguliwa tarehe 16 Agosti 2018 na Mhe. Dkt. Joseph Butore Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Burundi, katika viwanja vya Sekondari vya SOS jijini Burundi na kuhudhuriwa na viongozi na watendaji waserikali kutoka nchi wanachama. 

Meza kuu ni Mhe. Dkt. Joseph Butore Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Burundi (wa pili kulia) Bw.Liberatus Mfumukeko (wapili kushoto)  Katibu Mkuu Seretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ali Kirunda Kivenjija Naibu wa Pili wa Waziri Mkuu na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki kutoka Uganda (wa kwanza kulia) na Mhe. Jacques Enyenimigabo Waziri wa Vijana na Michezo wa Burundi (wa kwanza kushoto) wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Burundi ukipigwa kwenye hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Kwanza la Michezo la Afrika Mashariki

Sehemu ya watendaji na viongozi wa Serikali wa nchi Wanachama wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Burundi ukipigwa kwenye ufunguzi wa Tamasha la Michezo

Wanamichezo kutoka Tanzania wakipita kwa furaha mbele ya jukwaa kuu kwenye hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Kwanza la Michezo la Afrika Mashariki

Moja ya mchezo wa ufunguzi wa tamasha ukiwa unaneendelea jijini Bujumbura, Burundi

Hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Kwanza Michezo la Afrika Mashariki ikiwa inaendelea

Bw. Liberatus Mfumukeko Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki akihutubia kwenye hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Kwanza la Michezo la Afrika Mashariki linaloendelea jijini Bujumbura, Burundi.
Loading...

No comments: