Tigo Pesa Yamwaga Mamilioni Kwa Mawakala Wake - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, July 18, 2018

Tigo Pesa Yamwaga Mamilioni Kwa Mawakala Wake


Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani – George Lugata (kushoto) pamoja na Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa – Restituta Kedmond wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni iliyohusisha mawakala 73,000 wa Tigo pesa nchini kote. Tigo imetoa zawadi za mamilioni ya pesa na bonasi kwa mawakala wake nchini kote katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani – George Lugata (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano kwa Said Khatib wa Mkunazini, Zanzibar aliyeibuka kama mshindi wa jumla katika promosheni iliyohusisha mawakala 73,000 wa Tigo pesa nchini kote. Tigo imetoa zawadi za mamilioni ya pesa na bonasi kwa mawakala wake nchini kote katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa, Restituta Kedmond.
…………………
Mawakala 12 wajinyakulia mamilioni ya pesa huku wengine lukuki wakipata bonasi kemkem katika promosheni
Dar es Salaam, 14 Juni, 2018.
Tigo Tanzania, kampuni inayoongoza kwa huduma za fedha kwa njia ya mtandao kupitia huduma yake ya Tigo Pesa, leo imewazawadia wakala wake 12 kutoka sehemu mbali mbali za nchi mamilioni ya pesa kama shukrani kwa utendaji wao mzuri.
Katika promosheni iliyohusisha mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo Pesa nchini kote, Tigo imetoa zawadi kwa washindi watatu wa kitaifa na washindi wengine watatu kutoka kila moja ya kanda nne za Tigo nchini.
Said Khatib Wakala wa Tigo Pesa wa eneo la Mkunazini, Zanzibar ndiye aliibuka kinara wa kitaifa na kujinyakulia TSH 5 milioni katika promosheni hiyo ‘Nawashukuru Tigo kwa kuwa mtandao unaowajali mawakala wao, kwani Tigo wanajitahidi kusikiliza na kushughulikia changamoto tunazozipata mawakala na kutupa mafunzo ya mara kwa mara yanayotusaidia kuenedana na hali halisi ya biashara hii,’ Said alisema.
Mshindi wa pili kitaifa aliyejinyakulia kitita cha shilingi 3 milioni ni wakala wa Duka la RBB lililopo Sinza, Dar es Salaam, huku Mojelwa Mlinga Mojelwa wa Pugu Dar es Salaam akiondoka na kitita cha shilingi 2 milioni kutoka Tigo Pesa. ‘Kupitia promosheni hii, Tigo wamethibitisha kuwa ni mtandao unaowajali sio wateja wake tu, bali pia mawakala na watoa huduma kwa ujumla. Kwani mitandao mingine huwa inaenedesha promosheni inayolenga wateja pekee yake, ila Tigo wametukumbuka mawakala na kutupa fursa ya kuongeza mitaji yetu,’ Mojelwa alisema.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani – George Lugata alisema kuwa lengo kuu la promosheni hiyo ilikuwa ni kuwarudishia shukrani mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo Pesa walioshiriki katika promosheni hiyo kote nchini. “Ningependa kuwapongeza mawakala wetu wote kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhakikisha kuwa huduma za kifedha zinapatikana kwa urahisi kwa watu wote kote nchini,’ alisema.
Washindi wa kanda katika promosheni hiyo walipata zawadi za shilingi milioni mbili, shilingi milioni moja na shilingi laki tano kila mmoja, huku maelfu ya mawakala wakijishindia bonasi kemkem.
Tigo ni kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini na inatoa huduma bora za kipekee za sauti, SMS na intaneti ya kasi ya juu ya 4G inayopatikana katika miji 24 nchini kote. Tigo pia inafahamika kwa promosheni kabambe na ofa bunifu kwa wateja wake. Tigo Pesa ni huduma ya fedha ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini.
Loading...

No comments: