WAZIRI LUGOLA AAGIZA ZITTO KABWE KUJISALIMISHA KATIKA KITUO CHA POLISI

Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola ameagiza mbunge wa kigoma mjini Zitto Kabwe kujisalimisha kwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi kwa madai kuwa amekufanya mkuatano katika jimbo lisilokuwa lake pamoja na kutoa kauli za uchochezi.
Waziri Lugola amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari nakusema kuwa Zitto alifanya uchochezi huo wakati alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la kilwa kusini.
Katika hatua nyingine waziri Lugola  baada ya mazungumzo na mmiliki wa kampuni ya Lugumi Said Lugumi amempa miezi minne kukamilisha kufunga vifaa vya utambuzi wa alama za vidole kwenye baadhi ya vituo vya polisi na katika jeshi la polisi
Kampuni ya Lugumi iliingia mkataba wa shilingi billion 37 na jeshi la polisi kufunga mashine za kielektroniki zakuchukua alama za vidole katika vituo vya Jeshi Hilo, lakini ilibainika kutotimiza masharti baada ya kufunga mashine 14 kati ya 106 licha yakulipwa asilimia 90 ya fedha, kwa mujibu wa mkataba.


Na Amos C Nyanduku

Post a Comment

0 Comments