BENKI YA CBA NCHINI TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA 10 TANGU KUANZISHA KWAKE, SERENA JIJINI DAR ES SALAAM - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, September 10, 2018

BENKI YA CBA NCHINI TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA 10 TANGU KUANZISHA KWAKE, SERENA JIJINI DAR ES SALAAM

  Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Miaka kumi ya Benki ya Commercial Bank of Africa (CBA Bank) Nchini Tanzania Dkt. Reginald Mengi, Mwenyekiti  Mtendaji wa Kampuni ya IPP, akitoa hotuba yake ambapo alianza kusema kuwa ni muhimu kuamini kuwa unaweza bila kushindwa , aliongeza kuwa anaamini  Benki ya CBA hapo mbeleni itakuwa ya kwanza kwa kutoa huduma bora Tanzania,Afrika na duniani kwa ujumla,alipongeza menejimenti na wafanyakazi wa Benki ya CBA kwa huduma nzuri wanazotoa, bidhaa zao pamoja na kuwajali wateja wao wakubwa kwa wadogo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania Bw. Gift Shoko akitoa salam za shukurani na kuwakaribisha wageni mbalimbali katika sherehe ya maadhimisho ya miaka kumi ya Benki hiyo tangu ianzishwe nchini Tanzania, alisema kuwa wanajivunia kwa kuwa na huduma bora za kibenki ambazo wateja wengi wanafurahia mfano Mpawa, Private Banking, end to end solution na Mortgage Finance. Aliongeza kuwa benki inahuduma nzuri ambazo mteja akizipata ni ngumu kwake kuhama, mwisho aliwasihi wale wote ambao hawajiunga na Benki ya CBA wafanye hivyo.
Bw. Martin A. Mugambi ambaye ni 'Group Executive Director' wa Benki ya CBA ambaye pamoja na salam zake alianza kusema kuwa bila wateja basi Benki ya CBA haiwezi kwenda mbele, aliwashukuru wafanyakazi, wateja na watu wote waliohudhuria katika sherehe hiyo kwa kuendelea kuiamini Benki ya CBA. Alisema mpaka sasa Benki ya CBA ina zaidi ya wateja milioni 35 na bado wanaendelea kuongezeka zaidi. Alimalizia kwa kuwasihi wateja waendelee kufurahia huduma zao na mambo mazuri zaidi yanakuja.
Mmoja wa mashuhuda Mhandisi  Allan Makame akitoa ushuhuda wake wa namna Benki ya CBA iliyoweza kumsaidia na kukua naye tangu anaanza biashara zake mpaka sasa sasa amekuwa na kipato kikubwa zaidi, alifurahi kuwa miongoni mwa watu ambao wamekuwa na Benki hiyo tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania Miaka 10 iliyopita.
Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel taasisi inayojihusisha na kuwasaidia watoto Njiti, Bi. Doris Mollel ambaye na yeye pia alizaliwa akiwa Njiti akitoa shukurani zake za dhati kwa Benki ya CBA kwa kuendelea kumsaidia katika shughuli zake za kila siku za kuwasaidia watoto njiti ili waweze kukuwa na kufurahia maisha yao ya baade.
Mshereheshaji katika maadhimisho ya Miaka miaka kumi ya Benki ya CBA Mchekeshaji Maarufu Tanzania Bw. Evance Bukuku akiendelea kusherehesha 
Mgeni Rasmi katika sherehe za maadhimisho ya Miaka kumi ya Benki ya CBA Tanzania Dkt. Reginald Mengi (wa pili kushoto mstari wa chini) akiwa katika picha ya pamoja na wadau walionunua picha pamoja na kinyago kwa ajili ya kuwasaidia watoto njiti kupitia taasisi ya Doris Mollel.
 Meza kuu wakifurahia jambo
 Washindi mbalimbali walioshinda katika nafasi tofauti wakati wakicheza mchezo wa Golf wakichukua zawadi zao
 Mshindi wa Pili katika Mchezo wa Golf ambao ulichezwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kutimiza Miaka 10 ya Benki ya CBA akikabidhiwa zawadi yake na Mgeni Rasmi Dkt. Reginald Mengi
 Mshindi wa kwanza  katika Mchezo wa Golf ambao ulichezwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kutimiza Miaka 10 ya Benki ya CBA akikabidhiwa zawadi yake na Mgeni Rasmi Dkt. Regnald Mengi
 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Barnaba akitumbuiza mwimbo maalum wa kuipongeza Benki ya CBA kwa kutimiza Miaka 10 tangu ilipo anza hapa Dar es Salaam
 Msanii wa Muziki Banana Zoro akiwa pamoja na bendi yake wakitumbuiza wakati wa maadhimisho ya Miaka kumi ya Benki ya CBA Tanzania.
 Burudani ikiendelea 
 Mchezo wa Golf ukiendelea wakati wa maadhimisho ya Miaka kumi ya Benki ya CBA
 Baadhi ya wadau wakendelea kucheza mchezo huo hii ikiwa ni sehemu ya kwanza
 Mkurugenzi Mkuu wa CBA Bank Bw. Gift Shoko nchini Tanzania  (wa pili kulia aliyevaa tshirt nyeupe) akisikiliza jambo wakati mchezo wa Golf unaendelea.
 Mkurugenzi Mkuu wa CBA Bank Bw. Gift Shoko nchini Tanzania akianza kucheza Golf katika viwanja vya Gymkhana hii ikiwa ni hatua ya kwanza
  Mkurugenzi Mkuu wa CBA Bank Bw. Gift Shoko nchini Tanzania akendelea kucheza Golf katika hatua ya pili, kabla ya hapo akiongea na waandishi wa Habari katika viwanja hivyo alisema kuwa wameamua kusherekea na wacheza Golf wengine kwa sababu wao wamekuwa mstari wa mbele sana katika kuufadhiri mchezo huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CBA nchini Kenya Bw.Jeremy Ngunze akiendelea kucheza mchezo wa Golf katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar.
 Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa wanaendelea kujiandaa kucheza mchezo wa Golf katika viwanja vya Gymghana jijini Dar es Salaam
Picha na Fredy Njeje


Loading...

No comments: