Bondia kutoka Tanzania Jonas Segu ‘Black Mamba’ amefanikiwa kushinda Ubingwa wa WBF Africa Lightweight Champion Siku ya Jana baada ya kumpiga Bondia David Rajuili kutoka Afrika kusini katika pambano liliopigwa Mjini Cape Town.
Huu ni muendelezo mzuri kwa wanamasumbwi wa Tanzania kufanya vema katika mapambano ya nje ya nchii, ikikumbukwa kuwa majuma kadhaa yaliyopita Hassan Mwakinyo aliibuka na ushindi wa TKO baada ya kumpiga Muingereza mwenye kiwango cha juu kabisa duniani, Sam Egginton nakupanda hadi nafasi ya 16 katika pambano la ufunguzi lilofanyika England na kuiletea sifa kubwa Taifa.