CCM YAPONGEZA MAENDELEO YA UJENZI WA RELI YA KISASA (STANDARD GAUGE) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, September 27, 2018

CCM YAPONGEZA MAENDELEO YA UJENZI WA RELI YA KISASA (STANDARD GAUGE)

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndugu Masanja Kadogosa (kushoto) akimuelezea Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole (kulia) maendeleo ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa wakati wa ziara kuona maendeleo ya ujenzi wa SGR nje kidogo ya kambi ya Soga Kibaha mkoani Pwani Septemba 26, 2018.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Mhandisi Maizo Mgedzi akiwaelezea, Katibu wa Itikadi na Uendezi wa CCM Humphrey Polepole, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC Prof. John Kondoro, Mkurugenzi Mkuu wa TRC ndugu Masanja Kadogosa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Bi. Kate Kamba kuhusu maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la treni ya Umeme linalojengwa kuanzia Stesheni ya ¬Dar es Salaam hadi Ilala Septemba 26, 2018.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa ziara kuona maendeleo ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR nje kidogo ya kambi ya Soga Kibaha Septemba 26, 2018.
Mhandisi kutoka kampuni ya Yapi Merkezi akiwaelezea Katibu wa Itikadi na Uendezi wa CCM Humphrey Polepole, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC Prof. John Kondoro, Mkurugenzi Mkuu wa TRC ndugu Masanja Kadogosa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Bi. Kate Kamba kuhusu hatua za ujenzi wa daraja la treni ya umeme linalojengwa kuanzia Dar es Salaam Stesheni hadi Ilala Septemba 26, 2018.


Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepongeza maendeleo ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge inayoendelea kujengwa kwa awamu ya kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.

Mwaka 2015, CCM iliweka ahadi kwa Wananchi wake kuimarisha, kuboresha na kuiunda upya Miundombinu ya Usafirishaji nchini ikijumuisha Usafiri wa Ardhini na Ndege.

Akizungumza wakati wakutembelea maendeleo ya ujenzi wa Reli hiyo eneo la Soga mkoani Pwani, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema kukamilika kwa kipande hicho (Dar hadi Morogoro) itasukuma malengo ya dira ya maendeleo ya Taifa mwaka 2020/2025 kufikia Uchumi wa Kati.

Polepole amesema Reli ni kiungo muhimu kuchochea Taifa la Tanzania kufika katika Uchumi wa Kati wenye sifa ya wingi wa Viwanda vitakavyoongeza ajira kwa vijana.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Ramadhan Maneno amesema Chama hicho kimefika katika eneo hilo la Pwani kuthibitisha ujenzi wa Reli hiyo iliyoahidiwa mwaka 2015, amesema Mkoa wa Pwani umetoa ushirikiano kwa Kampuni ya Yapi Merkezi kutoka Uturuki ambayo imechukua tenda ya ujenzi wa Reli hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema wamepata faraja kwa ujumbe wa CCM kufika katika eneo la Pwani kutembelea ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa. "Tuna Wataalamu 57 Wanajeshi maeneo mbalimbali ya Ujenzi wa Reli hii, tunafarijika sana", amsema Kadogosa.

Pia Kadogosa ametoa wito, Wataalamu wanaoendelea na ujenzi wa Reli hiyo kutoka hapa nchini watapata mafunzo ya vitendo kusomea nje ya nchi, amesema mapaka sasa Reli hiyo imetandikwa zaidi ya Urefu wa Kilometa 5 akisisitiza kuwa Reli zilizofika ni Kilometa 60.

Akizungumza kwa niaba ya Bodi ya Shirika la Reli nchini, Prof. John Kondoro amesema kuna watu wanafaidika na uwepo wa Kampuni zinazotengeneza Reli ya Kisasa, pamoja na maendeleo ya ujenzi wake.Prof Kondoro amesema hadi kufika mwisho wa mwaka lengo ni kuondoa miinuko na mabonde ili kufanikisha utandikaji wa Reli hiyo.


Loading...

No comments: