DC awatangazia kiama wavamizi wa misitu - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, September 24, 2018

DC awatangazia kiama wavamizi wa misitu


Kulia ni Meneja Misitu ya Hifadhi wilayani Biharamulo Emmanuel Komba akimweleza Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Dos Santos Silayo (aliyeshika kiuno) jinsi wavamizi wa maeneo ya msitu wa Nyantakara wilayani humo wanavyathiri uhifadhi na kuhujumu uchumi wa Taifa walipotembelea situ huo na kujionea uharibifu mkubwa wa msitu huo unaosababishwa na shughuli za uchomaji mkaa . Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mhe. Sada Malunde
Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mhe. Sada Malunde (mwenye kofia) akiwataka wananchi wote wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya hifadhi ya Biharamulo na msitu wa Nyantakara wilayani humo kuondoka mara moja kabla ya kuwachukulia hatua za kisheria alipokuwa kwenye Kijiji cha Mpago kilichopo ndani ya msitu wa Nyantakara wilayani Biharamulo jana. Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Professa Dos Santos Silayo mwenye dhamana ya kusimamia msitu huo.
Mmoja kati ya wavamizi wa msitu (hakuweza kufahamika jina lake) wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika msitu wa Nyantakara wilayani Biharamulo akiendelea na shughuli zake katika msitu huo licha ya kutakiwa kuondoka mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria kama alivyokutwa na mpiga picha wetu katika Kijiji cha Nyamagana kilichopo ndani ya msitu huo.


Loading...

No comments: