IDADI YA WATU WALIOFARIKI KWENYE KIVUKO CHA MV NYERERE YAONGEZEKA NA KUFIKIA 79 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, September 21, 2018

IDADI YA WATU WALIOFARIKI KWENYE KIVUKO CHA MV NYERERE YAONGEZEKA NA KUFIKIA 79


 Miili ya watu 79 tayari imeopolewa hadi kufikia asubuhi ya leo Septemba 21, 2018, kufuatia kupinduka kwa kivuko cha MV Nyerere mika 100 kutoka maegesho ya Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza na zoezi la uokoaji linaendelea. Inadaiwa kivuko hicho kilikuwa kimebeba watu zaidi ya 100 wengi wao wakitoka kwenye mnada wa Bugorora.


Habari za awali-

WATU 14 wameripotiwa kufa maji na wengine 32 kuokolewa kufutia kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya visiwa vya Bugorora na Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa Televisheni ya Taifa (TBC1), ajali hiyo imetokea leo Septemba 20, 2018 majira ya saa 8 mchana ambapo uchunguzi wa awali unaonyesha kivuko hicho kilikuwa kimebeba kupita kiasi na kwamba hadi ajali hiyo inatokea kilikuwa umbali wa mita 100 tu kufika kwenye maegesho ya kisiwa cha Ukara.
Habari nyingine zinasema kuwa, kuzama kwa kivuko hicho kun aweza kuchangiwa pia na haraka za abiria kutaka kushuka kwani kivuko hicho kilikuwa kinakaribia kufika na kwamba abiria walianza kusogea mbele ili waweze kushuka haraka pindi kivuko kitakapotia nanga na hivyo kupelekea uzito kuelemea upande mmoja na kufanya kipinduke.
Taarifa zaidi zinasema kuwa Alhamisi huwa panafanyika mnada huko Bugurora na kwamba leo hii kulikuwa na abiria wengi.
Wakala wa Ufundi wa umeme TEMESA, umethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwaomba wananchi kuwa watulivu wakati taarifa zaidi zikiendelea kukusanywa.
Wakati huo huo Mkurugezni wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bw. Gerson Msigwa, amesema Rais John Mgufuli ametoa salamu za pole kufuatia vifo  vya watu hao na wale wote walionusurika na wanaendelea kupata matibabu na kuwataka Watanzania kuwa watulivu wakati serikali kupitia vyombo vyake vinaendelea na uokoaji. Taarifa hiyo ya Msigwa imesema, Rais amepokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella kuwa hadi sasa  maiti 44 zimepatikana na zoezi la uokoaji litaendelea t
Loading...

No comments: