JKCI YAWAALIKA WAHARIRI, WAANDISHI NA WATOTO WAO KUFANYIWA UCHUNHGUZI WA MARADHI YA MOYO BURE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, September 27, 2018

JKCI YAWAALIKA WAHARIRI, WAANDISHI NA WATOTO WAO KUFANYIWA UCHUNHGUZI WA MARADHI YA MOYO BURETAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha Wahariri na Waandishi wa Habari kwamba katika kuadhimisha siku ya moyo Duniani kutafanya uzinduzi wa upimaji wa afya ambao utaenda sambamba na upimaji na utoaji wa elimu ya afya ya moyo bila malipo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari wote pamoja na watoto wao.

 Kwa mujibu wa taarifa ya JKCI iliyotolewa leo asubuhi Septemba 27, 2018, upimaji huo utafanyika Ijumaa, tarehe 28/09/2018 kuanzia saa nne (4) asubuhi katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.

 Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya moyo Duniani inasema: “Kwa moyo wangu, kwa moyo wako, sote pamoja kwa mioyo yetu , tunatimiza ahadi”.
Wakati huo huo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha wananchi kwamba  itafanya  upimaji na utoaji wa elimu ya afya ya moyo bila malipo katika  Hospitali ya Vijibweni iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Upimaji huu utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia saa 2 (mbili) asubuhi. Wananchi wote mnakaribishwa.
Loading...

No comments: