Kikwete, Mkapa na Mwinyi Walivyosherehekea miaka 20 ya Balozi wa Marekani - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, September 12, 2018

Kikwete, Mkapa na Mwinyi Walivyosherehekea miaka 20 ya Balozi wa MarekaniBalozi mstaafu wa Marekani nchini Tanzania wakati wa utawala wa Serikali ya awamu ya tatu chini ya Benjamin Mkapa, Balozi Charles Stith amesema anajisikia faraja kusherehekea miaka 20 ya ubalozi nchini kutokana na mapenzi mema na nchi ya Tanzania.
Balozi Charles amesema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 20 ya ubalozi ambapo maraisi wastafu mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Dk.Jakaya Kikwete walishiriki kwenye sherehe hiyo.

Mbali ya marais wastaafu, wakati wa sherehe hiyo viongozi wengine wa ngazi mbalimbali pamoja na wageni waalikwa wakiwemo baadhi ya madaktari bingwa kutoka Marekani pia  walishiriki.
  
Balozi Stith alisema akiwa balozi kati ya mwaka 1998 hadi mwaka 2001 amepata ushirikiano mkubwa kwa Rais mstaafu Mkapa huku Rais mstaafu Dk.Kikwete wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Amemshukuru Mkapa na Kikwete kwa ushirikiano ambao walikuwa wakimpatia katika kuhakikisha uhusiano wa nchi hizo unaendelea na kwamba akiwa nchini Tanzania amefanikisha kuingiwa kwa makubaliano mbalimbali yenye tija kwa nchi za Afrika na hasa Tanzania.
  
“Nimefurahi kuja Tanzania kukutana na kusheherekea miaka 20 ya Ubalozi.Nimefurahi kumuona Rais mstaafu Mwinyi,Rais mstaafu Mkapa na Rais mstaafu Kikwete.Tulishirikiana na tunaendelea kushirikiana,” Alisema Balozi Stith.

Loading...

No comments: