Mkurugenzi wa M-Commerce
wa Vodacom Tanzania Ashtosh Tiwary (kulia) akikabidhi funguo za gari kwa
Lucy Sarah Ismail (wa pili kulia) mshindi wa 10 wa gari za kampeni ya
m-pesa wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka kumi ya m-pesa jijini
Dar es Salaam wikiendi hii. Wengine ni Mkurugenzi wa mawasiliano na
uhusiano wa Vodacom, Rosalynn Mworia (wa pili kushoto) na Alec Mulonga
Mkurugenzi wa Mtandao wa Vodacom (kushoto).
Mkurugenzi
wa mawasiliano na uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia
akimuwashia gari Lucy Sarah Ismail, mshindi wa gari ya kumi wa kampeni
ya M-pesa aliyokabidhiwa jijini Dar es salaam wikiendi hii.
Mkurugenzi wa mawasiliano na uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kati)
akikabidhi funguo na hati ya gari kwa Lucy Sarah Ismail (kushoto),
mshindi wa gari ya kumi ya kampeni ya Mpesa aliyo kabidhiwa jijini Dar
es Salaam wikiendi hii. Kulia ni Mkurugenzi wa M-Commerce wa Vodacom,
Ashtosh Tiwary.
Dar es Salaam, Tanzania Katika maadhimisho ya kuanzishwa kwa huduma ya
M-Pesa ya Vodacom nchini,kampuni ya Vodacom Tanzania imekabidhi gari la mwisho
aina ya Renault KWID 2017 kwa Lucy Sarah Ismail mkazi wa Dar es Salaam ambaye
ni mshindi wa mwisho katika kampeni ya kipindi cha wiki 10, ambayo imewezesha
washindi 10 kujishindia magari mapya
aina ya Renault KWID na fedha taslimu shilingi milioni 120/- kampeni hiyo iliwahusisha
wafanyakazi,mawakala na wateja.
Shamrashamra
hizo za kusherekea, zilizodumu kwa
kipindi cha wiki 10, zililenga kuwashukuru zaidi ya wateja milioni 8.2
wanaotumia huduma ya M-Pesa, ambao walishuhudia ikianzishwa kutoka huduma za
kifedha kupitia simu za mkononi kwa kufanya mihamala ya kutuma fedha na
kutumika kulipia huduma muhimu katika
maisha ya kila siku, ikiwemo huduma za kibenki kupitia mtandao wa simu za
mkononi,kuweka akiba na kukopa na kuaminika kutumika kufanya mihamala ya malipo
ya kimataifa.Mpaka sasa biashara au mtoa
huduma ambaye hakubali kutumia huduma ya M-Pesa atabaki nyuma kibiashara.
Akiongea
katika hafla ya kukabidhi gari la mwisho,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom
Tanzania,Hisham Hendi,alibainisha kuhusu mapinduzi yaliyoletwa na matumizi ya
huduma za fedha kupitia simu za mkononi nchini Tanzania, “Matumizi ya
teknolojia yamewezesha kuogezeka kwa kiasi kikubwa cha matumizi ya huduma ya
M-Pesa kwa kuwezesha asilimia 55% ya wananchi kupata huduma za kifedha.Tunatambua
safari hii ndefu katika historia ya kampuni yetu na mchango mkubwa kutoka kwa
wateja wetu,mawakala na wabia wengine tulioshirikiana nao kupata mafanikio ya
huduma ya M-Pesa nchini Tanzania-na tuendelee kutarajia
mambo mengine mazuri yatakuja”.
M-Pesa imefanikisha na inaendelea
kuwa na mchango mkubwa kwa uchumi ambapo
asilimia 37 ya mzunguko wa fedha katika Pato la Taifa hupitia
katika M-Pesa kila siku, imewezesha
ajira zaidi ya 200,000 na zaidi ya biashara 20,000 hufanya mihamala mbalimbali kupitia M-Pesa
kila siku. Kutokana na manufaa yake katika kukuza uchumi tutaendelea kufanya
ubunifu wa kiteknolojia kwa kuiboresha zaidi ili wateja wazidi kuifurahia
sambamba na kuimarisha ubora wa huduma zetu.
Mapema mwaka huu, huduma za M-Pesa
zimethibitishwa na GSMA kuwa ina usalama mkubwa na kutangazwa katika ngazi ya
dunia kuwa huduma ya kwanza kupata hadhi hiyo. Mapema wiki hii, Jumatatu tarehe
10.9.2018, ilizindua kadi ya kwanza ya mtandao nchini Tanzania-Kadi hiyo ya
M-Pesa imezinduliwa kwa ushirikiano wa MasterCard na Benki ya BancABC ambayo
inaruhusu wateja kufanya mihamala ya malipo kupitia mtandaoni kwenye biasharaza
ndani na kimataifa kwa usalamana urahisi.Uzinduzi huu wa hivi karibuni umekuja
katika kipindi cha muda mfupi kuanzisha programu ya kufanya mihamala ya malipo
ya QR katika matumizi ya huduma za M-Pesa.
Hishamu alimalizia kwa kusema, “Wateja
wetu ni moyo wa kila kitu tunachofanya na ndiyo sababu tunafurahi kuwa katika
safari hii na Watanzania tukiwa tunaongoza kuipeleka nchi katika ulimwengu wa
kidigitali kupitia ubunifu mkubwa wa matumizi ya mtandao, sio tu kwa kwa huduma
za M-Pesa bali kuunganishwa katika mtandao wetu ulio na ubora mkubwa.
No comments:
Post a Comment