MC LUVANDA APANDISHWA KIZIMBANI KUJIBU TUHUMA TATU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, September 24, 2018

MC LUVANDA APANDISHWA KIZIMBANI KUJIBU TUHUMA TATUMtuhumiwa Anthony Luvanda maarufu kama MC Luvanda akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiwa amejifunika usoni leo jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko,blogu ya Jamii.
MSHEHERESHAJI maarufu nchini,Anthony Luvanda maarufu kama MC Luvanda pamoja na kampuni yake,amepandishwa katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu likiwemo la kutumia kikoa ambacho akijasajiliwa Tanzania.

Luvanda anashtakiwa pia kwa kutoa maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Mbali na luvanda washtakiwa wengine waliofikishwa mahakamani hapo Leo Septemba 24 kwa makosa kama hayo mbele ya mahakimu watatu tofauti ni pamoja na Fadhili Kondo, Michael Mligwa na kampuni ya Luvanda ya Home of Company Limited.

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yanayowakabili mahakamani hapo kwa nyakati tofauti mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, 
Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na Hakimu Mkazi Mkuu, Hamza Wanjah 

Akimsomea mashtaka MC Luvanda, wakili wa Serikali Mkuu, Tumain Kweka amedai mbele ya Hakimu Shaidi kuwa mfanyabiashara MC Luvanda na kampuni anayomiliki ya Home of Company Limited walitumia kikoa ambacho akijasajiliwa Tanzania.

Amedai kati ya Februari 24 na Septemba 2018 katika jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa alianzisha na kutumia mtandao wa www.mcluvanda.com ambao haukuwa na kikoa cha .tz.

Pia imedaiwa katika kipindi hicho mshtakiwa alianzisha na kutumia mtandao huo ambao haukuwa na kikoa cha .tz.
Aidha imedaiwa,mshtakiwa huyo alitoa Huduma ya online bila ya kuwa na kibali.

Mc Luvanda anadaiwa kuwa katika kipindi hicho alitoa huduma hiyo kupitia online TV ifahamikayo kama MC Luvanda pasipokuwa na kibali toka TCRA.

Mshtakiwa Luvanda amekana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Wakili Jebra Kambole anayemtetea mshtakiwa huyo aliiomba mahakama itoe dhamana kwa mteja wake kwa sababu shtaka linadhaminika.

Akisoma masharti ya dhamana, hakimu Shaidi alimtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja Mwenye barua na kitambulisho ambaye atasaini bondi ya Sh 5 milioni.

Mshtakiwa huyo alifanikiwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana na kuachiwa huru. 
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 23, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Kwa upande wa mshtakiwa, Michael Mlingwa ambaye ni mpiga picha amepandishwa katika kizimba cha mahakama ya hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba akikabiliwa na shtaka la kutumia mtandao bila kusajiliwa na TCRA.

Akimsomea mashtaka mshtakiwa huyo Wakili wa Serikali, Faraja Nguka alidai kuwa mshtakiwa huyo katika kipindi hicho cha Februari 24 mwaka huu jijini Dar es Salaam kinyume cha sheria alimiliki na kutumia mtandao wa WWW.Slidevisual. Com bila leni kutoka TCRA. 

Mshtakiwa amekana mashtaka na yuko nje kwa dhamana yenye masharti ya kuwa na wadhamini wawili, waliosaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 10. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba nane kwa ajili ya kutajwa.

Mshtakiwa mwingine John Lusingu amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hamza Wanjah kwa shtaka la kutumia mtandao waWWW.magazetini.com bila leseni. 

Mshtakiwa amekana mashtaka hayo anayodaiwa kuyatenda Februari 24 na Septemba mwaka huu, yuko nje kwa dhamana hadi Oktoba. 5,mwaka huu
Washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana.

Kwa Hisani ya Michuzi Blog
Loading...

No comments: