MJUKUU WA MALKIA WA UINGEREZA PRINCE WILLIAM APOKEWA NA WAZIRI DKT. KIGWANGALLA NA PROF KABUDI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, September 26, 2018

MJUKUU WA MALKIA WA UINGEREZA PRINCE WILLIAM APOKEWA NA WAZIRI DKT. KIGWANGALLA NA PROF KABUDINA ANDREW CHALE, DAR

MJUKUU wa Malkia wa Uingereza, Prnce William ametua Nchini Tanzania jioni ya Septemba 26, 2018 na kupokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla, na Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi, kwenye uwanja wa ndege wa Kiamtaifa wa Julius Nyerere.

Prince Williamkwa atakuwa nchini kwa ziara maalum ya siku tatu ambapo leo Septemba 27,  2018 anatarajiwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es Salaam.

Prince William katika kukutana na Rais Magufuli atafanya mashauriano kuhusu juhudi zinazochukuliwa na Tanzania katika kukabiliana na ujangili na ulanguzi wa wanyama pori.

Kwa mujibu wa ratiba ya Mwanamfalme huyo, baada ya mkutano wake na Rais Magufuli, atatembelea bandari ya Dar es Salaam kuangalia juhudi za upanuzi wa bandari hiyo ili kuondoa msongamano wa meli na mizigo, lakini pia  atatembelea kitengo cha askari wanamaji (Marine Polisi Unit) lakini pia atatembelea eneo la kupokelea mizigo, upekuzi na ukaguzi wa mizigo inayoingia na kutoka nchini.

Pia Prince William anatarajiwa kukutana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo Mpingo Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Prince William na ugeni wake huo unatarajiwa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na baadae Chuo cha Wanyamapori cha Mwika (College of African Wildlife Management, Mwika (CAWM), kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro na kisha kuendelea na ziara yake Nchini Kenya.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa lengo kuu ya ziara hiyo ya Prince William ni pamoja na kufuatilia juhudi za kukabiliana na ujangili na uhifadhi wa wanyama.

Prince William atafanya ziara hiyo katika wadhifa wake kama rais wa mashirika yanayotetea uhifadhi wa wanyama ya United for Wildlife na Tusk Trust. Amekuwa pia mlezi wa shirika la Royal African Society linalolenga kukuza uhusiano kati ya Afrika na Uingereza na hushiriki sana juhudi za kukabiliana na ujangili.
Loading...

No comments: