Mjukuu wa mfalme Prince William atembelea hifadhi ya taifa ya Mkomazi nchini Tanzania na ajifunza haya - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, September 29, 2018

Mjukuu wa mfalme Prince William atembelea hifadhi ya taifa ya Mkomazi nchini Tanzania na ajifunza haya

Mjukuu wa mfalme wa Uingereza Prince William ambaye ziara yake ilianza sptember 24 akitembelea nchi tatu Tanzania Kenya pamoja na Namibia tayari yuko nchini Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi ambazo ziko kwenye ziara yake ambayo ni ya siku saba ikitarajiwa kumalizika september 30.
Dhumuni kubwa kabisa la mjukuu huyo wa mfalme ni kufuatilia juhudi za kukabiliana na ujangili na uhifadhi wa wanyama. Prince William atafanya ziara hiyo katika wadhifa wake kama rais wa mashirika yanayotetea uhifadhi wa wanyama ya United for Wildlife na Tusk Trust. Amekuwa pia mlezi wa shirika la Royal African Society linalolenga kukuza uhusiano kati ya Afrika na Uingereza na hushiriki sana juhudi za kukabiliana na ujangili.
Kwa sasa Prince William tayari yuko katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kujifunza zaidi juu juhudi zinzofanywa na hifadhi hiyo za kuhakikisha kuwalinda Vifaru weusi pamoja na kuwatengenezea mazingira ya kuzaliana zaidi.Lakini pia akiwa Mkomazi alifanikiwa kuona jinsi hifadhi hiyo inavyofanya kazi katika  kuwatunza na kuwatengenezea mazingira mazuri vifaru wazaliane kwani tayari kuna vifaru weusi 50,na kupitia vifaru hao inafanya juhudi mbalimbali za kuhakikisha vifaru wengine wanaongezeka zaidi,ikidaiwa Vifaru wanapotea na kupungua kutokana na ujangili lakini pia kulingana na ongezeko la watu nchini Tanzania.
Loading...

No comments: