OXFAM WAKUTANA NA WADAU KUJADILI MIKAKATI YA KUKABILIANA NA MAJANGA. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, September 19, 2018

OXFAM WAKUTANA NA WADAU KUJADILI MIKAKATI YA KUKABILIANA NA MAJANGA.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la kimataifa la Oxfam Nchini Tanzania Bw. Francis Odokorach akitoa neno la utangulizi  na maelezo machache juu ya Mkutano  na wadau kuhusu kujadili mikakati ya kukabiliana na majanga uliofanyika Hoteli ya Seashells jijini Dar es Salaam.
Bi. Magdalen Nandawula akielezea kwa ufupi kuhusu malengo ya kukutana kujadili kuhusu kukabilia na Majanga.
Bw. Pieter akielezea kwa kwa kina  kuhusu malengo ya kukutana kujadili kuhusu kukabilia na Majanga.

Shirika la Kimataifa la Oxfam Nchini Tanzania limejipanga katika kutafuta njia mbadala zitakazosaidia kupambana na maafa mbalimbali nchini ili kupunguza athari zake pale zitakapojitokeza

Maafa  hayo yaliyotajwa ni pamoja na mafuriko na ukame ambayo yamekuwa yakijitokeza katika maeneo mbalimbali yameingizwa katika mpango wa dharura wa miaka miwili

Mratibu wa mradi wa kukabiliana na Majanga (DDR) ), Bw. Yangai Ole Mkulago, akizungumza katika mkutano huo ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Oxfam alisema kuwa kuna haja ya kuwa na mikakati ya kitaifa itakayopunguza maafa hayo na kuwa jitihada kubwa zinaelekezwa katika kuhakikisha kuna njia mbadala za kupunguza ama kuzuia kabisa maafa hayo.

Aliongeza kuwa kwa sasa jitihada kubwa zinaelekezwa katika kuhakikisha kunakuwa na njia madhubuti za kupunguza ama kuzuia kabisa athari za maafa kipindi cha kabla hayajatokea.

"Tuko hapa kwa lengo la kutengeneza mkakati wa Kitaifa kwaajili ya kukabiliana na majanga ambayo yamekuwa yakitokea hasa kwenye Wilaya ambazo zimekuwa zikikubwa na ukame na mafuriko,"amesema.

Kwa sasa mradi huo umeanza kutekelezwa katika mikoa miwili ambayo ni kigoma katika Wilaya ya kibondo na Shinyanga katika Wilaya za Kahama na Kishapu.

Aliongeza "Oxfam kama mdau wa maendeleo  tunajitahidi kuangalia tunakuwa na mkakati kwaajili ya kukabiliana na changamoto zinapotokea," .

Kwa upande wake Ofisa Mradi wa DDR Bw. Projestus Mwemezi amesema mradi huo umejikita zaidi katika maeneo matatu  ambayo ambapo ni pamoja na kuhakikisha wanatoa uelewa kwa wanajamii juu ya mambo mazima yanayohusu maafa ili waweze kujikinga pindi yanapotokea

"Kamati za Maafa katika ngazi ya Wilaya zimekuwa zikisuasua kutekeleza majukumu yake na kwamba mradi huo umelenga pia kuziwezesha ili ziweze kusimama" alisema

Aliongeza kuwa ,Sheria yetu namba Saba ya mwaka 2015  inaelezea namna ya kujiandaa kukabiliana na maafa lakini tumekuwa tukikabiliana na maafa pale tu yanapotokea.

Hatua moja wapo ambayo Oxfam imeanza kutekeleza ni pamoja na utoaji wa simu za mkononi katika kamati hizo ili ziweze kusaidia kutoa taarifa za maafa mapema kwa wahusika ili hatua za mapema ziweze kuimarika. Mpango huo utakamilika ifikapo mwaka 2020
Loading...

No comments: