RC MAKONDA AWAAGIZA WAKUU WA WILAYA KUSIMAMIA SUALA LA LISHE. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, September 24, 2018

RC MAKONDA AWAAGIZA WAKUU WA WILAYA KUSIMAMIA SUALA LA LISHE.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaagiza Wakuu wa Wilaya kuweka mkazo na kusimamia ipasavyo suala la lishe katika maeneo yao na kufanya Mkoa huo kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwa na wakazi wenye afya bora.
RC Makonda amesema hayo leo wakati wa kikao cha utilianaji saini wa mkataba wa lishe baina yake na Wakuu wa Wilaya ambapo amesema suala la lishe duni limekuwa tatizo kubwa linalopelekea matatizo ya uwezo mdogo wa kufikiri, udumavu, utapia mlo, idadi ya watoto njiti, watoto wanaozaliwa na mgongo wazi, vichwa vikubwa, uono hafifu, ukosefu wa damu, vitamin na tatizo la ukondefu.
Aidha RC Makonda amesema Mkoa umejidhatiti kukabiliana na tatizo la lishe kwa kutoa elimu ya lishe, kuzuia magonjwa ya upungufu wa viini lishe, kuongeza virutubisho kwenye chakula pamoja na matibabu ya utapiamlo.
Pamoja na hayo RC Makonda amesema takwimu za lishe Mkoa wa Dar es salaam Mwaka 2015 zinaonyesha 14.6% sawa na watoto 91,000  kati ya watoto 624,000 wana Utapiamlo (udumavu) sugu, 4.7% sawa na watoto 23,000 wana Ukondefu, 59.5% sawa na watoto 371,000 wenye umri chini ya miaka 5 wana upungufu wa damu na 53.3% sawa na kinamama walio kwenye umri wa kuzaa 330,000 wana upungufu wa Damu hali inayoonyesha kuwa kuna kazi kubwa ya kufanya kukabiliana na tatizo la lishe duni.
Kwa mujibu wa wataalamu wa Afya athari za kudumu za ukosefu wa Lishe hutokea siku 1,000 za kwanza kuanzia wakati wa ujauzito hadi pale mtoto anapotimiza umri wa miaka miwili.

ACN

Loading...

No comments: