Ronaldo awapongeza Salah na Modric baada ya kufanikiwa kushinda tuzo kupitia simu yake - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, September 29, 2018

Ronaldo awapongeza Salah na Modric baada ya kufanikiwa kushinda tuzo kupitia simu yake


Mchezaji wa klabu ya Juventus na taifa la Ureno Cristiano Ronaldo ameweza kutoa kauli yake baada ya kimya kidogo kutokana na kutofanikiwa kupokea tuzo yeyote zilizotolewa London siku ya jumanne ya wiki iliyopita baada ya kushinda Mo Salah akimbwaga Ronaldo na Bale kwenye kipengele cha goli bora lakini pia katika kipengele cha mchezaji bora wa mwaka wa FIFA akishinda Luca Modric kwa mara ya kwanza.

Ronaldo alitumia video ndogo ambayo ilitumwa kwenye mitandao ya kijamii akianza kwa kumsifia Mmisri na mchezaji wa Liverpool Mo Salah akisema ” Salah alistahili mana alifunga goli zuri huku akimsifia pia Modric na kusema hongereni kwa wote”
Katika tuzo hizo ambazo zilitolewa katika jiji la London nchini Uingereza wachezaji wawili nguli sana duniani Ronaldo pamoja na Messi hawakufanikiwa kufika katika hafla hiyo huku wadau na wachezaji mbalimbali wakiwalaumu wachezaji hao kwa kutohudhuria.
Licha ya Ronaldo kutokupokea tuzo yeyote katika tuzo hizo za FFA lakini pia hakuweza kushinda tuzo zingine zinazotolewa na UEFA ambazo zilifanyika Monaco,ambapo Modric alifanikiwa kushinda pia katika tuzo hizo.
Tuzo pekee ambayo inayosubiriwa kwa hamu sana ni tuzo ya Ballon d’or ambapo Ronaldo yote tena kwenye kipengele cha mchezaji bora wa mwaka,huku yeye na Muargentina ndio wanaoongoza kushinda tuzo hizi wakishinda kwa nyakati tano tofauti tofauti kila mmoja.
Loading...

No comments: