Samatta aiweka wazi ndoto yake ya kumilikia ndege binafsi ( Private Jet) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, September 12, 2018

Samatta aiweka wazi ndoto yake ya kumilikia ndege binafsi ( Private Jet)

Mchezaji wa klabu KRC Genk kutoka nchini Ubelgiji na taifa la Tanzania Mbwana Ally Samatta ameamua kuiweka wazi ndoto yake ya kumiliki chombo cha Usafiri ndege.
Samatta ameamua kuiweka ndoto yake hiyo baada ya kupiga picha katika ndege ya klabu yake ya KRC Genk nje ya mlango wa kuingilia na kuandika haya.
Ikumbukwe mchezaji huyo anafanya vizuri sana katika klabu yake hiyo baada ya kung’ara katika michezo ya kufuzu kucheza UEFA europa League,baada ya kuisadia klabu yake hiyo kufuzu katika michuano hiyo.
Lakini pia amekuwa tegemezi sana katika klabu hiyo na hata timu ya taifa lake Taifa stars,ingawa juzi aliweka wazi ligi gani anatamani kuichezea bila kujali atachezea katika klabu gani ila kwanza aichezee tu ligi hiyo ambayo aliitaja kama ligi kuu nchini Uingereza alimaarufu EPL.Samatta alisema ” Natamani sana kucheza katika ligi kuu ya Uingereza sitojali ni timu gani ila tu nichezee ligi hiyo ndio ndoto zangu”
Mpaka sasa Samatta amevitumikia vilabu vitatu ambavyo ni Simba ya Tanzania ,TP Mazembe ya Congo na KRC Genk y Ubelgji ambayo alijiunga nayo mwaka 2016 akiichezea michezo 66 na kuifungia magoli 19 tu.
By Ally Juma.KWA HISANI YA BONGO5.COM
Loading...

No comments: