SERIKALI YAJIPANGA KUIFANYA SEKTA YA MADINI KUCHANGIA ZAIDI YA ASILIMIA 10 KATIKA PATO LA TAIFA IFIKAPO 2025 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, September 27, 2018

SERIKALI YAJIPANGA KUIFANYA SEKTA YA MADINI KUCHANGIA ZAIDI YA ASILIMIA 10 KATIKA PATO LA TAIFA IFIKAPO 2025Naibu Waziri Wizara ya Madini Mhe. Stansalus Nyongo akiongea wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho Teknolojia na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita, ambapo alisisitiza kuwa Ifikapo 2025 Sekta ya Madini Ichangie zaidi ya asilimia 10 katika pato la taifa.
NA MWANDISHI WETU-MAELEZO, GEITA
SERIKALI imesema itahakikisha mpaka kufikia mwaka 2025 Sekta ya madini iwe inachangia zaidi ya asilimia 10 katika pato la taifa. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stanslaus Nyongo wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Teknolojia bora ya dhahabu tarehe 26/09/2018 Mkoani Geita.
Mhe. Nyongo amesema kuwa katika mwaka 2016/2017 sekta ya madini imechangia asilimia nne tu katika pato la taifa hivyo hii imechagiza serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha wanafikia zaidi ya asilimia 10 ifikapo 2025. “kwa ujumla sekta ya madini imekuwa ikitoa mchango mkubwa sana katika uchumi wa taifa letu na maendeleo ya mtu mmojammoja nchini ingawa matarajio ya Serikali ni mchango huu kuongezeka zaidi na hatimaye kuinufaisha zaidi nchi na watanzania kwa ujumla”-Alisema Mhe. Nyongo. Aidha, Mhe. Nyongo amesema kuwa mbali na mchango huo Serikali itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Jiolojia Tanzania na kuendelea kutoa ushirikiano kwa wachimbaji wadogo ili kuhakikisha wanafikia lengo lililotarajiwa ikiwemo kuwawekea mazingira mazuri ya utekelezaji majukumu yao. Mhe. Nyongo amesema kuwa Wizara ya madini itashirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Geita ili kuhakikisha kunakuwepo na soko la madini katika eneo hilo. Pia Mhe. Nyongo aliwataka wachimbaji wadogo wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu za sekta ya madini  na kuacha kujihusisha na utoroshaji wa madini au kufanya biashara ya magendo ikiwemo kukwepa mrabaha na kodi za serikali kwani kufanya hivyo ni kuihujumu nchi. Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwa mtetezi namba moja katika sekta ya madini ili yawanufaishe watanzania. Mhandisi Gabriel amesema kuwa anaishukuru serikali kwa kuzuia kaboni kusafirishwa nje ya mkoa kwani baada ya katazo katika mwezi wa sita walipata kilo 115.8, kwa mwezi wa saba walipata kilo 141 ya dhahabu na kwa mwezi wa nane wamepata kilo 157.4, tofauti na miezi ya nyumba kabla ya katazo hilo hii imewezesha halmashauri kupata fedha yake na Serikali kuu kukusanya kodi. Akiongea katika mkutano huo Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amewathibitishi wananchi kuwa Serikali ya awamu ya tano ipo kazini na kuna mambo yanatokea nchi hii hayajawahi kutokea tangu Tanzania iumbwe.
  Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho Teknolojia na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita ambapo alisisitiza Serikali ya awamu ya tano itaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

  Naibu Waziri Wizara ya Madini Mhe. Stansalus Nyongo akitembelea baadhi ya mabanda katika maonesho Teknolojia na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita.

  Naibu Waziri Wizara ya Madini Mhe. Stansalus Nyongo akitembelea baadhi ya mabanda katika maonesho Teknolojia na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita.

  Naibu Waziri Wizara ya Madini Mhe. Stansalus Nyongo akitembelea baadhi ya mabanda katika maonesho Teknolojia na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita.

  Naibu Waziri Wizara ya Madini Mhe. Stansalus Nyongo akiongea wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho Teknolojia na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita, ambapo alisisitiza kuwa Ifikapo 2025 Sekta ya Madini Ichangie zaidi ya asilimia 10 katika pato la taifa.

  Naibu Waziri Wizara ya Madini Mhe. Stansalus Nyongo akiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi rasmi wa maonesho Teknolojia na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita
Loading...

No comments: