#UBER;Usalama kuanzia Mwanzoni, Mambo Tunayofanya Nyuma ya Pazia Wakati wa Kuandikisha Dereva-Mshirika - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, September 6, 2018

#UBER;Usalama kuanzia Mwanzoni, Mambo Tunayofanya Nyuma ya Pazia Wakati wa Kuandikisha Dereva-Mshirika
Kampuni ya Uber imewekeza sana katka teknolojia ambayo imeiwezesha kuweka kipaumbele kwenye usalama wa wasafiri na madereva kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho: kabla msafiri hajaabiri gari, wakati wote wa safari, na baada ya kufika mahali anakoenda. Kuanzia pale mchakato mzima wa kumwandikisha dereva na kuweka magari kwenye mfumo wa Uber, kuna masharti ambayo yanamtaka dereva mshirika kuweka nyaraka muhimu ambazo zinasaidia sana katika kulinda usalama wakati wa matumizi wa mfumo wetu. Kadhalika Uber ina mpango wenye wigo mpana unaotoa huduma kwa wateja wetu usiku na mchana kupitia Timu ya Matukio ya Dharura na tunafanya semina elekezi endelevu zinazowajengea uwezo madereva washirika ili kuimarisha usalama wa mfumo huu.

Masharti ya Kuwa Dereva Jijini Dar es Salaam
•   Vigezo na Masharti ya Kuwa Dereva:
  • Leseni ya Dereva (Class C, C1, C2, C3): Madereva wote wanaotumia app ya Uber sharti wawe wameandikisha magari yao kwa shughuli za biashara na wawe na leseni ya dereva ya kibiashara
  • Uchunguzi wa Tabia Njema ya Dereva: Madereva wote lazima wapiti mchakato wa uchunguzi wa tabia kabla ya kuruhusiwa kutumia app ya Uber. Mchakato huu unahusu kuleta cheti cha tabia njema kutoka jeshi la polisi kinachotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani.
  • Semina za mafunzo: Madereva wote wanatakiwa kufanya kozi maalum inayotolewa katika ofisi zetu za VKituo cha Dereva wa Uber, baada ya kuhitimu, akaunti ya dereva mshirika itaruhusiwa kutumia app ya Ube. Kadhalika, madereva washirika wanatakiwa kuhakikisha kwamba wanahudhuria vikao vyote ambavyo vinatumiwa na Uber kuwapa mafunzo zaidi kuhusu namna ya kuboresha huduma wanayotoa kwa abiria. Vikao hivi pia hutumika kutoa maelezo ya kina kuhusu Miongozo ya Jamii ya Uber, ambayo inaelezea kwa uwazi kabisa viwango ambavyo vimewekwa na Uber na kusistiza tabia ambayo hairuhusiwi na tabia inayoruhususiwa dereva anapokuwa akitumia app ya Uber sambamba na vitendo vinavyoweza kusababisha dereva na msafiri kunyimwa uwezo wa kutumia app ya Uber.

•   Magari:
  • Kadi ya Usajili wa Gari la Biashara:  Magari yote sharti yawe na kadi inayoonyesha kwamba yamesajiliwa kwa shughuli za biashara inayotolewa na Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA)
  • Bima:  Magari yote yanayotumia mfumo wa Uber sharti yawe na bima ya magari ya biashara na bima ya ulinzi wa umma.  
  • Stika: Madereva wanaotumia Uber jijini Dar es Salaam wanatakiwa wapewe stika itakayowatambua kama dereva wa Uber kutoka kwa halmashauri ya jiji la Dar es salaam.  
•   Usaidizi wa Madereva-Washirika:
  • IRT: Timu yetu ya Matukio ya Dharura (IRT) iko tayari kukupa usaidizi wowote usiku na mchana siku zote za wiki watakusaidia katika matukio yoyote ya dharura au ajali.  
  • Namba za simu za Dharua: Kampuni ya Uber imeingia ubia na kampuni ya SGA Security, kampuni ya ulinzi ya humu nchini ili kuwapa madereva namba za simu wanazoweza kutumia kupiga simu wakati wowote wanapokuwa na dharura.

Loading...

No comments: