TANZIA: John Guninita wa CCM Afariki Dunia - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, September 13, 2018

TANZIA: John Guninita wa CCM Afariki Dunia


Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Dar es Salaam John Guninita amefariki dunia.

Taarifa zinabainisha kuwa Guninita ambaye ameshawahi kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM), alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na mdogo wake na marehemu, Gerald Guninita ambaye naye aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo wakati wa Uongozi wa Awamu ya Nne.

Miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015, Guninita alikuwa miongoni mwa makada wa CCM waliojiunga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kupewa cheo cha meneja wa kampeni.

Hata hivyo, mapema mwaka huu, marehemu Guninita aliripotiwa kurudi CCM huku akiomba radhi kwa hatua yake ya kukihama chama alichokitumikia kwa muda mrefu.
Loading...

No comments: