Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa akimuonesha Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (wa nne kulia) na Naibu Waziri
wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia) namna
kazi ya utandikaji reli ya kisasa ya SGR inavyofanyika kwenye eneo la Soga mkoa
wa Pwani
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (wa tatu kulia)
akipata maelezo ya namna ya kutengeneza mataruma ya reli ya kisasa ya SGR
kwenye kIiwanda cha Soga, Pwani. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa na wa kawanza kushoto ni Farid Munir
Abdallah, Mhandisi Mzalishaji wa Kampuni ya Yapi Merkezi
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (aliyeketi kushoto)
na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
(aliyechuchumaa) wakizindua kazi ya kutandika reli ya kisasa ya SGR kwenye eneo
la Soga, Pwani. Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli
Tanzania, Masanja Kadogosa
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati) akikagua
kipande kilichotandikwa reli ya kisasa ya SGR, Soga mkoani Pwani. Kulia kwake
ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye na
kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa
Mmoja
wa mafundi wakiendelea na kazi ya kutengeneza mataruma ya kujengea reli ya
kisasa ya SGR kwenye iwanda cha Soga kilichopo mkoa wa Pwani
No comments:
Post a Comment