VODACOM YAINGIA MAKUBALIANO MAPYA NA GOOGLE PLAY STORE KURAHISISHA UNUNUZI WA APP


 
 Mkuu wa Mawasiliano na Mahusiano ya umma wa Vodacom, Jacquiline Materu (kati) akiwaonesha waandishi wa habari jinsi ya kufanya manunuzi  kwa kutumia salio la simu wakati wa uzinduzi wa ubia huo kati ya Vodacom na Google Play Store jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni  Meneja wa Ushirikiano wa Jukwaa la Android Afrika kutoka GoogleCassandra Mensah-Abrampah (kulia) na Mtendaji wa huduma za thamani wa Vodacom, Prestin Lyatonga (kushoto)

 Mkuu wa Mawasiliano na Mahusiano ya umma wa Vodacom, Jacquiline Materu akizungumza na  waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ubia kati ya Vodacom Tanzania na Google Play Store unaorahisisha manunuzi kwa kutumia salio la simu jijini Dar es Salaam leo. 
 
 Meneja wa Ushirikiano wa Jukwaa la Android Afrika kutoka GoogleCassandra Mensah-Abrampah (kulia) akizungumza na waandishi wakati wa uzinduzi wa ubia kati ya Vodacom Tanzania na Google Play store unaorahisisha manunuzi kwenye Google Play Store. Wengine ni  Mkuu wa Mawasiliano na Mahusiano ya umma wa Vodacom, Jacquiline Materu (kati) na Mtendaji wa huduma za thamani wa Vodacom, Prestin Lyatonga(kushoto)

 Mtendaji wa huduma za thamani wa Vodacom, Prestin Lyatonga (kati) akimuonesha Francis Kajubi jinsi ya kununua kitabu kwenye google play store kwa kutumia salio lake la simu. Kulia ni Meneja wa Ushirikiano wa Jukwaa la Android Afrika kutoka GoogleCassandra Mensah-Abrampah.
Mkuu wa Mawasiliano na Mahusiano ya umma wa Vodacom, Jacquiline Materu akiwaonesha waandishi wa habari jinsi ya kupakua zana kwa kutumia salio la simu wakati wa uzinduzi wa ubia huo kati ya Vodacom na Google Play Store jijini Dar es Salaam leo. 
September 12,2018 .Mtandao wa simu unaongoza nchini, Vodacom Tanzania PLC leo imetangaza makubaliano na Google ili kuwapa wateja wake fursa ya kununua maudhui mbali mbali kwenye Google Play store kwa kutumia salio la simu. Huduma hii, ambayo  inapatikana kwa wateja wote wa Vodacom wenye vifaa au simu za Android, inawezesha ununuzi wa programu mbali mbali kwenye Google Play Store kwa kutumia salio la simu kwenye mtandao wa Voda.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa umma, Bi. Jacquiline Materu alisema: "Kwa kuwa Mtandao wa 4G superfast wa VODACOM una kidhi, tunafurahi kushirikiana na Google kuleta njia hii rahisi, nyepesi na ya kuaminika ya malipo kwenye  Google Play Store  kwa ajili ya ununuzi wa app ama programu mbali mbali kwa Watanzania. Hii ina imarisha zaidi azimio yetu ya kuzidi kuwakaribisha wateja wetu katika ulimwengu wa kidijitali huku tukiwapatia urahisi na thamani kutokana na matumizi ya kadi za benki kwa ajili ya kufanya manunuzi mtandaoni kuwa mdogo sana hapa nchini.

Sasa wateja wa Vodacom wenye vifaa ama simu za Android wataweza kununua maudhui katika Google Play Store, kama programu za michezo,filamu, maonesho ya TV na vitabu vya kielekroniki kwa urahisi zaidi, kwa kutumia salio la simu kweye mtandao wa voda. Hapo awali ni kadi za benki ndizo zilikuwa zinatumika kufanya manunuzi hayo 
 
Materu aliendelea kufafanua kuwa, uvumbuzi huu unarahisisha mchakato wa malipo na kuboresha huduma kwa wateja wake, “kama jukwaa la kuwasilisha maudhui, tumebeba jukumu la kutaarifu, kuelimisha na kuburudisha wateja wetu kwakutumia teknolojia, aliongeza kuwa wamepiga hatua kubwa kuwezesha jukwaa mbalimbali za kidijitali na kijamii kuweza kupatikana kirahisi zaidi kwenye mtandao huku wakitengeneza mifumo ya kidijitali yenye kujumuisha kila mtu”
 
Pembeni yake Cassandra Mensah-Abrampah, Meneja wa ushirikiano wa jukwaa la Android|Afrika kutoka Google, alisema "Tunafurahi sana kuongeza wigo wa ushirikiano wa malipo ya moja kwa moja baina ya Google Play Direct na Vodacom Group ikiwa ni pamoja na kufanya uzinduzi huu na Vodacom Tanania. Utoaji kwa njia ya simu ni mojawapo ya nguzo muhimu kwenye ujumuishi wa kifedha katika uchumi wa app ama programu katika masoko kwa sababu watu wengi bado hawana akaunti za Benki"  

Wateja watakaopenda kutumia njia hii bora ya malipo wanahitaji kufanya ifuatavyo: Ingia kwenye Google Play Store> Chagua content (Games/Apps or Movies) nenda kwenye Buy option> kisha chagua Vodacom Airtime billing as mode of payment, kisha utahitajika kuingiza taarifa zako binafsi na kuendelea na malipo baada ya kuthibitishwa. Hatua hizi zinahitajika tu kwa ununuzi wa kwanza tu. Malipo mengine yote yatakuwa ni ya moja kwa moja baada ya kuchagua mfumo wa malipo wa kutumia salio la simu kwenye mtandao wa Voda.


Post a Comment

0 Comments