Waanzilishi wa Instagram wajiuzulu ‘Ni miaka nane sasa toka kuanzisha mtandao huu’ - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, September 25, 2018

Waanzilishi wa Instagram wajiuzulu ‘Ni miaka nane sasa toka kuanzisha mtandao huu’


Waanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Kevin Systrom na Mike Krieger wameamua kujiuzulu nafasi zao ili kwenda kuanzisha ubunifu mwingine.
Kevin Systrom (R) and Mike Krieger
Kevin Systrom (kushoto) na Mike Krieger walikuwa kwenye bodi ya usimamizi hata baada ya Facebook kununua mwaka 2012.
Systrom ambaye amekuwa mkurugenzi mkuu mtendaji wa Instagram tangu kuasisiwa amesema wanajiondoa kwenye nafasi walizokuwa nazo chini ya Facebook ilikufufua ubunifu wao upya.
Wawili hao walisalia katika bodi ya usimamizi wa Instagram hata baada ya kununuliwa na Facebook mwaka wa 2012 kwa gharama ya dola bilioni moja
Mkurugenzi huyo mwenye umri wa miaka 34 na mwezake Krieger mwenye miaka 32, ambaye alikuwa ni mkuu wa kitengo cha maswala ya kiufundi walianza mtandao wao wa Instagram mwaka 2010 na hata kuendelea nao baada ya kumuuzia Facebook.
Mkurugenzi Mtendaji, Mark Zuckerberg amesema katika taarifa yake kuwa waanzilishi hao wa Instagram wamejaliwa vipaji na ubunifu.
“Nimejifunza mengi katika kufanya nao kazi kwa miaka sita iliyopita na nilifarijika sana, bado nasubiria kuona kitu gani kipya wanakuja nacho siku za usoni,’ amesema Mark Zuckerberg
Loading...

No comments: