WAZIRI MAHIGA AFUNGUA RASMI OFISI NDOGO ZA UWAKILISHI WA UBALOZI WA UJERUMANI JIJINI DODOMA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, September 14, 2018

WAZIRI MAHIGA AFUNGUA RASMI OFISI NDOGO ZA UWAKILISHI WA UBALOZI WA UJERUMANI JIJINI DODOMA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwa pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Detlef Waechter wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi Ndogo ya Uwakilishi wa Ubalozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani jijini Dodoma. Ofisi hiyo ni ya kwanza kwa Balozi za nje zilizopo Tanzania kufunguliwa Dodoma. Ufunguzi huo ni katika kuitikia wito wa Mhe. Rais baada ya Serikali kuhamia rasmi Dodoma. Ofisi hizo ambazo zipo ghorofa ya nne katika Jengo la PSPF Barabara ya Benjamin Mkapa zitatoa huduma mbalimbali kwa Serikali, Bunge na Wananchi kwa ujumla huku zikisimamiwa na Bw. Richard Shaba ambaye ni Mtanzania. Pia Ofisi hizo zimejumuisha Mashirika ya Misaada ya Ujerumani ambayo ni GIZ na KFW. 
Mhe. Waziri Mahiga kwa pamoja na Balozi Waechter wakifungua kitambaa kuashiria kuwa Ofisi Ndogo za Uwakilishi wa Ubalozi wa Ujerumani zimefunguliwa rasmi jijini Dodoma
Loading...

No comments: