DKT NDUGULILE AMEWAAGIZA WATENDAJI WA WIZARA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAKAZI YA WAZEE FUNGAFUNGA. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, October 22, 2018

DKT NDUGULILE AMEWAAGIZA WATENDAJI WA WIZARA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAKAZI YA WAZEE FUNGAFUNGA.


 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisalimiana wazee wanaoishi katika Makao ya Wazee ya Fungafunga yaliyoko katika Manispaa ya Morogoro wakati waziara yake mkoani  humo kujionea hali ya maisha ya Wazee hao wanaotunzwa na kusimamiwa na Wizara yake.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagu aeneo la makazi ya makao ya Wazee ya Fungafunga yaliyoko katika Manispaa ya Morogoro wakati waziara yake mkoani humo kujionea hali ya maisha ya Wazee hao wanaotunzwa na kusimamiwa na Wizara yake kushoto ni Kaimu afisa Mfawidhi wa Mkazi hayo Bw. Rashid Omari.
 
Wazee wanaoishi katika Makao ya Wazee ya Fungafunga yaliyoko katika Manispaa ya Morogoro wakimasikiliza Naibu Waziri wa  Afya, MaendeleoyaJamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipofika katika Makao yao wakati wa ziara yake mkoani humo kujionea hali ya maisha ya Wazee hao wanaotunzwa na kusimamiwa naWizara yake.
(Picha na WAMJW)
Naibu Waziri wa Afya, MaendeleoyaJamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wazee wanaoishi katika Makao ya Wazee ya Fungafunga yaliyoko katika Manispaa ya Morogoro wakati wa ziara yake mkoani humo kujionea hali ya maisha ya Wazee hao wanaotunzwa na kusimamiwa na Wizara yake.
Na Mwandishi Wetu Morogoro
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia Wazee,  na Watoto  Mhe.  Dkt Faustine Ndugulile amewaagiza watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia,  Wazee,  na Watoto upande wa Idara Kuu Maendeleo ya Jamii kushughulikia changamoto zinazokabili Makazi ya Wazee Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro Mkoani Morogoro.
Dkt. Ndugulile amemuagiza Katibu Mkuu  Maendeleo ya Jamii,  Jinsia,  Wazee na Watoto Dkt.  John Jingu kutatua changamoto hizo zilizolwasilishwa na Kaimu Mfawidhi wa Makazi hayo.
Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.  John Pombe Magufuli inawajali na kuwatunza wazee nchini kwani imedhamiria kuboresha huduma katika makazi ya wazee .
Dkt.  Ndugulile pia amewaagiza watendaji wa Wizara kufuatilia kwa ukaribu uratibu wa makazi ya wazee nchini kwa kuhakikisha wazee  ndio wananufaika na huduma zinazotolewa na Serikali  katika makazi ya Wazee na kuwaondoa wale wote wasiostahili kukaa katika makazi ya hayo.
Dkt. Ndugulile pia amesisitiza kuharakisha upimaji wa eneo la Makazi ya Wazee Fungafunga ambalo bado halijapimwa ili kuondoa migogoro ya ardhi inayoweza kujitokeza.
Akisoma maelezo kuhusu Makazi ya Wazee ya Fungafunga Kaimu Mfawidhi wa Kituo hicho Bw.Rashid Omari amesema kuwa Makazi hayo yanakabiriwa na changamoto nyingi  ambazo ni pamoja na ukosefu wa bwalo la wazee kula chakula na jiko la kisasa la kupikia pamoja na huduma bora za Afya kwa wazee.
Wakizungumza katika mkutano huo baadhi ya wazee wanaoishi katika makazi ya wazee fungafunga wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwajali wazee nchini.
Makazi ya wazee fungafunga ni miongoni mwa makazi 19 yanayomilikiwa na Serikali kwa lengo la kutoa huduma kwa wazee wasio na ndugu wala familia za kuwalea.
Loading...

No comments: