FID Q NA JUX WAACHA VIBE LA TIGO FIESTA MUSOMA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, October 30, 2018

FID Q NA JUX WAACHA VIBE LA TIGO FIESTA MUSOMA


Wasanii Fid Q na Jux usiku wa kuamkia jana waliacha alama ya Vibe la Tigo Fiesta  kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma.
Wasanii
hao kwa wakati tofauti wakiwa kwenye steji waliweza kuteka hisia za
mashabiki waliofurika uwanjani hapo. Msanii Fid Q ndiye aliyefungua
pazia la Tigo Fiesta mjini Musoma mkoani Mara, Kwa mkoa huo wasanii
wanaopendwa zaidi ni wa mtindo wa kufokafoka (Hip Hop) ndipo Fid Q
alipopewa jukumu la kuanza na kuamsha shangwe kubwa na hasa alipomaliza
kwa wimbo wake ujulikanao kama FRESH.

Nae Juma Jux ambaye ni
“Fundi” wa nyimbo Laini aliweza kuwaimbisha mashabiki mwanzo hadi mwisho
aliposhuka kwenye jukwaa hilo kwa nyimbo zake JUU, ZAIDI na UTANIUWA na
nyingine nyingi kwa kweli huyu ndio msanii aliyeweza kuimba na
mashabiki kwa pamoja.
Tamasha hilo linatarajiwa kuendelea mjini Muleba ijumaa hii kwenye uwanja wa Zimbihire.
 Msanii Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q akiwa kwenye jukwaa la Tamasha
la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Karume mjini
Musoma usiku wa kuamkia jumatatu.


Loading...

No comments: