HATIMAYE MO DEWJI APATIKANA AKIWA HAI, IGP SIRRO ATOA KARIPIO KALI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, October 20, 2018

HATIMAYE MO DEWJI APATIKANA AKIWA HAI, IGP SIRRO ATOA KARIPIO KALI


Mfanyabiashara mashuhuri barani Afrika Mohamed Dewj amepatikana akiwa hai baada ya kutekwa na watu wasiojulikana kwa siku 9 huku Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro akisema Jeshi lake bado linaendelea kuwasaka watu wote wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo.
Taarifa za kupatikana kwa Mfanyabiashara huyo zimeanza kuenea majira ya asubuhi ya Jumamosi October 20, mwaka huu, ambapo video ya awali ilimuonesha Mo akiwa na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salam Lazaro Mambosasa nyumbani kwake Oysterbay Jijini Dar es salaam.
Baada ya tukio hilo, ndipo IGP Simon Sirro akazungumza na waandishi wa habari katika eneo la Gymkana ambapo gari linalosadikiwa kutumiwa na watekaji wa Mfanyabiashara huyo limetelekezwa.
Kupatika kwa Mo Dewj kunamaliza Sintofahamu iliyogubika fikra na mioyo ya watanzania kwa takribani siku 9 ambazo mfanyabiashara huyo hakujulikana alipo na wala waliomteka.
NA Amos Nyanduku  ... ACN
Loading...

No comments: