JPM KULA CHAKULA CHA MCHANA NA TAIFA STARS IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, October 19, 2018

JPM KULA CHAKULA CHA MCHANA NA TAIFA STARS IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO


Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Ijumaa Oktoba 19, 2018 atakutana na wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ujumbe mfupi uliochapishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Gerson Msigwa kwenye ukurasa wake wa Instagram mapema leo asubuhi umesomeka hivi. "Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Oktoba, 2018 atakutana na wachezaji wa Timu ya Taifa (Taisa Stars) na baadaye kula nao chakula cha mchana Ikulu jijini Dar es Salaam". mwisho wa ujumbe huo wa Bw. Msigwa.
Mapema wiki hii, Taifa Stars iliichapa timu ya taifa ya Cape Verde kwa mabao 2-0 katika pambano la marudiano la michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON2019 nchini Cameroon. Kwa ushindi huo, Stars imechupa hadi nafasi ya pili baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 5 nyuma ya Uganda Cranes yenye pointi 10.
Stars imebakiza michezo miwili mmoja dhidi ya Lesotho mjini  Maseru na mchezo mwingine dhidi ya Uganda Cranes jijini Dar es Salaam. Wachambuzi wa soka wanasema kuna matumaini makubwa ya Taifa Stars kufuzu kucheza fainali hizo kutokana na ari kubwa waliyoionyesha wachezaji hao katika pambano la marudiano dhidi ya Cape Vrde, ambapo licha ya kuchapwa mabao 3-0 katika pambano la awali lililopigwa mjini Praya, Stars haikuvunjika moyo na ilipambana kufa na kupona kwa dakika zote 90 huku mashabiki wakionyesha kushangilia kwa nguvu.
Loading...

No comments: